Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Chama Cha ADA -TADEA Mhe. Juma Ali Khatib (kulia )akikabidhiwa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025 ya Chama hicho, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni iliyofanyika katika Viwanja vya Magirisi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo 15-9-2025 akikabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa ADA -TADEA Zanzibar pia ni Mgombewa Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Makame Issa (kushoto)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha ADA-TADEA Mhe. George Busungu akizungua wakati wa Ufunguzi wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Juma Ali Khatib na Wabunge,Wawakilishi na Madiwani, ufunguzi huo uliyofanyika katika viwanja Magirisi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja, kizungumzia Sera za Cha Chake kuwaombea Kura Mgombea Urais na Wabunge,Wawakilishi na Madiwani.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha ADA -TADEA Zanzibar pia ni Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Makame Issa , akizungumza na kunadi Sera za Chama Chake, kabla ya kumkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Chama chake Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Juma Ali Khatib, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani uliyofanyika katika viwanja vya Magirisi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.
Viongozi Wakuu wa Cha Cha ADA-TADEA wakiwa katika viwanja vya Magirisi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar, Wabunge,Wawakilishi na Madiwani.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Chama cha ADA-TADEA Mhe.Juma Ali Khatib akionesha Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2025 na Sera Fasaha na Itikadi ya Chama Chake baada ya kukabidhiwa, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni wa Chama hicho uliyofanyika katika Viwanja vya Magirisi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa Chama Cha ADA-TADEA Mhe. Juma Ali Khatib akisisitiza jambo wakati akitangaza Sera za Chama chake kwa Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Magirisi Wilaya ya Magharibi "B" Unguja, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kampeni uliyofanyika katika viwanja hivyo na kuomba Kura na kwa Wagombea wa Ubunge,Uwakilishi na Udiwani.
No comments:
Post a Comment