Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na kufanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Katika mkutano uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, mjumbe huyo maalum, Robinson Njeru Githae ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jiji la Nairobi, amemkabidhi Rais Kikwete ujumbe maalum kutoka kwa Rais Kibaki.
Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete na Waziri Githae wamezungumzia maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na jinsi ya kuboresha uhusiano huo.
Viongozi hao pia wamejadili maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na changamoto zinazoikabili Jumuia hiyo na jinsi Tanzania na kenya zinavyoweza kuchangia katika kuboresha mchakato wa kuongeza mshikamano baina ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Nchi wanachama wa EAC ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi
Teknolojia : Wizara Maji na Matumizi ya Teknolojia katika utatuzi wa
changamoto
-
Na: Dk. Reubeni Lumbagala
Wiki ya Maji Kitaifa nchini Tanzania na Siku ya Maji Duniani imemalizika
Machi 22, 2026. Imekuwa ni wiki nzuri kwani mijadal...
38 minutes ago
0 Comments