Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi Maendeleo na Mipango Omar Yussuf Mzee, akizungumza na Waandishi, wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na Maendeleo na Mafanikio ya Wizara yake katika Kipindi cha Mwaka mmoja. Mkutano huu umefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Vuga.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Fedha akitowa maelezo ya Mafanikio ya Wizara yake katika Kindi cha Mwaka mmoja.
Mwandishi wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Raya Hamad, akiulizia swali la Zanzibar inaingia katika mfumo wa Digitali, Vipi Wizara yake itaweza kupunguza ushuru kwa Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa hizo,ili mtu wa chini aweze kuvimudu na kwenda na wakati.na mfumo wa Digitali.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Habari Leo Khatib Suleiman,amneuliza swali la Zanzibar kuna Taasisi mbili za ulipaji Kodi yaani ZRB na TRA, ambazo zinafanya kazi moja ya kukusanya kodi. Serikali na mpango gani katika suala hilo?.
Mwandishi wa Gazeti la Zanzibar Leo Mwantanga Ame, akiuliza suali la mfuko wa Fedha za Muungano.
0 Comments