6/recent/ticker-posts

Kampuni ya VIGOR Yaidhamini Timu ya Chwaka Star.

 
Mkurugenzi Muendeshaji wa Makampuni ya Turky VIGOR Tofiq Salim Turkymwenye shati jeusi akimkabidhi Seti ya Jezi Mwakilishi wa Timu ya Chwaka Stars Issa Gavu na kulia Kocha wa timu ya Chwaka Stars, akikabidhiwa Jezi na Mkurugenzi wa Masoko wa Vigor Ahmeid Amir, Timu hiyo itakuwa chini ya Udhamini wa Kampuni hiyo ya VIGOR kwa muda wa miaka mitatu na Itajulkikana kwa Jina la VIGOR CHWAKA STAR.

Mkurugenzi wa Makampuni ya Turky VIGOR Tofiq Salim Turky, akimkabidhi seti ya jezi Kocha wa timu hiyo ya VIGOR CHWAKA STAR, ikiwa ni moja ya ufadhili wa kampuni hiyo kwa timu hiyo utakuwa kwa muda wa miaka mitatu itakuwa chini ya ufadhili wa kampuni hiyo kwa mahitaji yaote ya Vifaa vya michezo na gharama nyengine za timu hiyo.

Mkurugenzi wa Makampuni ya ya VIGOR Tofiq Salim Turky, akizungumza na Wachezaji na Wanachama wa timu ya Vigor Chwaka Star, ambayo ameidhamini timu hiyo kwa muda wa miaka 3, kuendeleza timu hiyo kufikia Ligi Kuu ya Zanzibar kwa sasa iko ligi Daraja la Pili, Udhamini huo utakuwa katika kuigharamia timu hiyo kwa kila kitu, makabidhiano hayo yamefanyika katika uwanja wa timu hiyo Chwaka.

Mwakilishi wa Chwaka Issa Gavu akitzungumza na kutoa shukrani kwa Kampuni ya VIGOR kutowa udhamini kwa timu yao na kutowa ahadi ya kufanya vizuri katika michuano ya ligi inayoshiri hivi sasa na kumuhakikishia timu hiyo itafanya vizuri na kupanda daraja hadi ligi kuu ya zanzibar kwa udhamini wake.

Wazee wa Vigor Chwaka Star wakimsikiliza Mdhamini wao alipofika kutowa shukrani na kuikabidhi seti ya jezi timu hiyo ili kuweza kushiriki ligi ya Wilaya ya Kati.
Kocha wa timu ya VIGOR Chwaka Star Mohammed Ali Itedi, akitowa shukrani kwa niaba ya Wachezaji wake na kuahidi kufanya vizuri katika michuano yao wakiwa chini ya udhamini wa Kampuni ya VIGOR. 
Mzee wa Timu ya Vigor Chwaka Star ambaye ni Sheha wa Chwaka Simai Msaraka, akitowa shukrani kwa Kampuni hiyo kukubali kuidhamini timu yao katika kipindi hichi kigumu timu yao ikikabiliwa na michuano ya ligi ya Wiala ya Kati na udhamini huo umefika wakati muafaka na kuahidi kushirikiana na Mdhamini huyu katika kuinua kiwango cha mchezo huo katika Kijiji cha Chwaka.


Wachezaji wa timu ya VIGOR Chwaka Star wakiwa katika mazoezi yao wakijiandaa na mchezo wa ligi ya Daraja la Pili Wilaya ya Kati.

Post a Comment

0 Comments