6/recent/ticker-posts

Sala ya Eid El Hajj yasaliwa Kijiji cha Marumbi Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.

 





Sheikh Rashid Ali Vuai,, akisalisha sala ya Eid El Hajjj katika viwanja vya mpira marumbi Wilaya ya Kati Unguja, Kitaifa sala ya Eid imesaliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa na Wananchi wa Jimbo la Chwaka.Kati Unguja
 Wananchi wa ilaya ya Kati wakihudhuria Ibadaa ya Sala ya Eid, wakisikiliza hutuba baada ya sala hiyo katika viwanja vya mpira marumbi wilaya ya Kati Unguja.


 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Kadhi Mkuuu wa Zanzibar Khamisi Haji , baada ya kumalizika kwa sala ya Eid iliosaliwa katika kijiji cha Marumbi Wilaya ya Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wananchi wa Marumbi baada ya Sala ya Eid kumalizika, kitaifa imefanyika katika Mkoa wa Kusuni Unguja katika kijiji cha Marumbi Wilaya ya Kati Unguja.

Post a Comment

0 Comments