Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka, akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM katika viwanja vya magereza tomondo, na kuwataka wapinzani kutokutumia, slogani za ASP, katika mikutano yao. Na kuwataka Vijana kupiga kura ya ndio wakati ukifika katika kura ya maoni ya Katiba iliopendekeza na Bunge la Katiba.
Viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Ndg Shaka Hamdu Shaka wqakati akimwaga sera za Chama cha Mapinduzi katika mkutano wa hadhara kukamilisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Omar Kinana katika Wilaya ya Dimani Kichama kutembelea miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Uchuguzi ya CCM kwa Wananchi wa Zanzibar.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mwakilishi wa jimbo la Chumbuni Mhe.Machano Othman, akizungumza katika mkutano huo na kuwataka Wananchi kuisoma Katiba na kuipigia kura ya Ndio katika kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika mwezi April 2015. na kutowa maelezo ya baadhi ya vipengele vya Katiba hiyo.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia wakati wa Viongozi wa CCM wakihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya magereza tomondo Unguja, na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdurahaman Omar Kinana katika viwanja hivyo, baada ya kumaliza ziara yake katika Mkoa wa Magharibi Wilaya Dimani.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Ali Karume, akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa historia ya Zanzibar ilikotoka hadi leo na kuwataka Wananchi kuipigia Kura ya Ndio Katiba Iliopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba, hii ni Katiba nzuri kwa maslahi ya Wananchi wa pande zote mbili za muungano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdurahaman Omar Kinana akimpongeza Balozi Ali Karume baada ya kumaliza kuzungumza na Wananchi wa Mkoa wa Magharibi Kichana katika viwanja vya magerza tomondo Unguja.
0 Comments