Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Ole kupitia CCM Nd. Mussa Ali Mussa wa mwanzo kutoka Kushoto akimfahamisha Mke wa Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibafr Mama Asha Suleiman Iddi hatua iliyofikia ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Vikunguni Chake chake baada ya juhudi kubwa alizochukuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kutakakukamilisha kituo hicho.
Kiongozi wa Vikundi vya Ushirika vya Kijiji cha Vikunguni Bibi Fatma Mohammed Ali akitoa Taarifa ya Vikundi hivyo mbele ya Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mamam Asha Suleiman Iddi aliyetembelea na kuaonana na Akina Mama wa Kijiji hicho.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza na akina Mama wa Kijiji cha Vikunguni Wilaya ya Chake chake.
Baadhi ya Akina Mama wa Kijiji cha Vikunguni Ewilaya ya Chake chake wakifuatilia hotuba ya Mama Asha wakati akizungumza nao pembezoni mwa Kituo cha Afya cha Kijiji hicho.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama
Asha Suleiman Iddi amesema
kwamba upo ulazima kwa akinamama Nchini kuchangamkia maisha na kuacha
tabia ya kusubiri akina Baba katika maamuzi ya familia kutokana
na mabadilido ya Dunia yaliyopo hivi sasa.
Alisema Akinamama wanapaswa kuelewa kwamba wao
ndio nguvu ya familia inayopaswa
kutafutiwa nyenzo na Mikakati mbali mbali ya kuendesha maisha
yao kila siku.
Mama Asha Suleiman Iddi alitoa kauli hiyo
wakati akizungumza na Akina Mama
pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Vikunguni mara baada ya kukagua Kituo cha
Afya cha Kijiji hicho kilimo ndani ya Sherhia ya Ng’ambwa Jimbo la
Ole Wilaya ya Chake chake Kisiwani Pemba.
Alisema uamuzi wao wa kuunda Vikundi vya
ushirika umekuja wakati muwafaka
kwa vile hakuna njia ya mkato ya kusaidia kujiongezea Kipato cha
kuwahudumia watoto wao hasa katika masuala ya Kielimu.
Mama Asha aliwanasihi akina Mama pamoja na
Wananachi wa Majimbo la Kisiwa
cha Pemba kuacha mazoea ya kuwapa madaraka Watu wasioniasahgihi
ya kuwasimamia katika maendeleo yao.
Alisema Viongozi wa Majimbo katika nafasi ya
Ubunge na Uwakilishi wametengewa
mifuko ya Jimbo iliyolenga kuwapa nguvu za kuwawezesha kuendesha
miradi ya Wananchi katika Maeneo yao lakini wengi kati yao wanashindwa
kusimamia kazi hiyo na badala yake kuhama kwenyen Majimbo yao mara
baada ya kuchaguliwa na Wananachi.
Mama Asha aliahidi kuvisaidia vikundi vya
Ushirika vya Kijiji cha Vikunguni
mara baada ya kukamilika kwa harakati za Uchaguzi Mkuu na kuwasisitiza
umuhimu wa kuendeleza Amani iliyopo Nchini.
Amesema Wananchi na hasa akina Mama Nchini
wanapaswa kuishukuru Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais wa Sasa Dr.Ali
Mohammed Shein kwa uamuzi wake wa kusimamia kwa nguvu zote amaniinayoendelea
kushamiri hivi sasa.
Mama Asha alifahamisha kwamba cheche ya vurugu
zinazoonekana kuashiriwa
hasa na Vijana katika baadhi ya maeneo nchini zinatokana na baadhi ya
Vijana wanaohusika na ishara hiyo kukosa ucha mungu.
Alieleza kwamba Imani ya Dini miongoni mwa
Wananchi hasa kundi hilo la Vijana
imepungua na kusababisha baadhi ya vijana kuwa na dalili ya maamuzi
ya kutaka kufanya fujo hatma yake inaweza kuitumbukiza Nchi katika
vurugu zisizo na ulazima wowote.
Mapema Kiongozi wa Vikundi vya Ushirika vua
Kijiji cha Vikunguni Bibi Fatma
Mohammed Ali alisema hadi sasa Kijiji hicho kimefanikiwa kuwa na Vikundi
vya Ushirika Vinne lakini kilichopata usajili ni Kikundi cha Jipe Moyo.
Bibi Fatma aliziomba taasisi zinazohusika
kusaidia elimu ya Ushirika itakayosaidia
kuviwezesha vikundi vilivyobakia vya Maslahi kwa Wote,Tujiendeleze
Mwanzo Mgumu kupata usajili wa kudumu na kuendeshashughuli
zao katika taratibu za kisheria zinazokubalika.
Alisema ili kuvijengea mazingira ya uzalishaji
vikundi hivyo umefika wakati
kwa Viongozi pamoja na Taasisi za fedha kutoa mikopo kwavikundi
hivyo mara baada ya kupata Taaluma inayokusudiwa ya kuendeshavikundi
hivyo.
Akitoa salamu katika hafla hiyo fupi Mkuu wa
Wilaya ya Chake chake Bibi
Hanuna Ibrahim Masoud alisema Kituo cha Afya cha Kijiji cha Vikunguni
kilichoanzishwa kwa Nguvu za Wananachi wenyewe kilipata msukumo
mkubwa katika ujenzi wake uliotolewa na aliyekuwa Mbunge wa eneo hilo
Mh. Hamad Rashid Mohammed.
Hata hivyo Bibi hanuna alisema jitihada hizo
zilipata changamoto kubwa ya
mvutano wa umiliki wa Kituo hicho kutoka kwa makundi mbali mbaliuliosababisha
uzoroteshaji wa ukamilishaji wa ujenzi wake.
Alisema mvutano huo ulichukuwa muda mrefu hali iliyopelekea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufika kusikiliza mzozo huo na kuwaahidi Wananachi wa Vikunguni kuwatafutia wafadhili wa kukamilisha ujenzi wa Kituo hicho.
Bibi Hanuna Ibrahim Masoud alifahamisha kwamba
juhudi za Balozi Seif zilipelekea
kupatikana kwa Kampuni ya Milele iliyokubali kusaidia kukamilisha
Ujenzi huo.
Alieleza kuwa Kampuni hiyo kwa nia ya kuunga
mkono jitihada za Wananchi
hao za kupata huduma za Afya ikajitolea pia kujenga Nyumba ya
Daktari sambamba na kufanya marekebisho makubwa zaidi ya ujenzi wa jengo la
Kituo hicho litakalokuwa na uwezo kamili wa kutoa huduma nyingi
zikiwemo zile la Akina Mama wajawazito na Watoto.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Chake chake kwa niaba ya
Wananachi wa Wilaya hiyo hasa
wale wa Kijiji husika cha Vikunguni alimpongeza Makamu wa ili wa
Rais wa Zanzibar kwa kukamilisha ahadi aliyotoa kwa Wananchi
hao wakati alipotenmbelea mwaka uliopita.
hao wakati alipotenmbelea mwaka uliopita.




0 Comments