6/recent/ticker-posts

Silaha za Maangamizi Zisiishie Mikononi mwa Makundi ya Kihalifu –Tanzania.

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzani katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, akichangia majadiliano kuhusu upokonyaji wa silaha na usalama wa kimataifa  mwishoni mwa wiki, ambapo ametoa wito wa jumuiya   ya kimataifa  kushirikiana katika kuhakikisha kuwa silaha za maangamizi haziishii mikononi mwa makundi ya kihalifu.

Na MwandishiMaalum, New York
 Tanzania imetoa wito Kwa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha inashirikiana kuhakikisha kwamba silaha za maangamizi zikiwamo za nyukilia haziangukii mikononi mwa makundi ya kihalifu.

Wito huo umetelewa mwishoni mwa wiki na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, wakati wa Mkutano kuhusu masuala ya uponyaji wa silaha na usalama wa kimataifa.

Katika mkutano huo wa kuzungumzia wengi walieleza wasiwasi wao kuwa ushirikiano wa karibu kati ya nchi ambazo zina silaha za nyukilia na zile ambazo hazina, lakini huku zile ambazo zinamiliki silaha hizo zikiendelea kuziboresha na kujilimbikizia.

“Ni jambo la kusikitisha, badala ya kuzipunguza silaha hizi na hatimaye kuzitokomeza kabisa,  nchi zinazomiliki silaha za nyukilia zinaendelea na kasi ya kuziboresha, kuzifufua na kujilimbikiza”. Akasema Balozi Manongi.

Akabainisha kuwa mbaya Zaidi hata zile nchi ambazo hazina 

silaha hizo nazo sasa zinatafuta kila maarifa ya kuwa nazo.

Jamba oambalo amesema ni tishio kwa usalama wa 

mwanadamu.

Amesisitiza kuwa ingawa ni miongo saba imekwisha kupita 

lakini madhara ya matukio ya Hiroshima na Nagasaki bado 

yanaendelea na yapo hai miongoni mwetu.

Balozi Manongi akaongeza kuwa ni muhimu basi 

utokomezaji wa silaha za nyukilia na teknolojia 
inayoambatana nazo likaendelea kupewa kipaumbele pamoja 
na kuwa na mikataba ya kisheria itakayosimamia jambo hilo.

Akasema kutokana na ongezeko la  ulimbikizaji wa silaha za nyukilia,  Jumuia ya kimataifa inawajibu wa kushirikiana kuhakikisha kwamba silaha hizo na nyingine za maangamizi haziangukii mikononi mwa makundi ya kigaidi na kihalifu.


Pamoja na ukweli kwamba silaha za nyukilia na zingine za maangamizi bado ni tishio kubwa kwa uhai wa mwanadamu.

Balozi Manongi akasema kwa nchi zinazoendelea tatizo la usambazaji na matumizi holela ya silaha ndogo na nyepesi zinaendelea kuwa janga kubwa kwa ustawi na maendeleo ya bara hili na kwingineko.

Akimnukuu Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa  Kofi Annan kwamba madhara yatokanayo na matumizi holela ya silaha ndogo na nyepesi yameendelea kuwa makubwa sana na madhara yake ni makubwa pengine kuzidi mabomu ya atomic yaliyoiangamizia  Hiroshima na  Nagasaki.

Akizungumzia zidi kuhusu matumizi holela ya silaha ndogo na nyepesi,   Mwakilishi huyo wa Tanzania  anasema mirindimo ya risasi na hata matumizi ya silaha kali zikiwamo za maangamizi,  haiwezi  au haitamhakikishia mwananchi maisha yenye hadhi, utu, ustawi na maendeleo.

Akasema kuna uhusiano mkubwa baina ya  Amani, usalama na utekelezaji wa Malengo ya maendeleo endelevu ya (Agenda 2030) malengo yanayojikita katika kumaliza umaskini pasipo kumwacha yoyote nyuma pamoja na kuilinda sayari ya dunia.
Akasema itakuwa vigumu kuyatekeleza malengo mapya ya maendeleo kama kiwango cha gharama za kujilimbikizia silaha kitaendelea ambapo inakadiriwa kuwa mataifa hasa yale makubwa yanatumia Zaidi ya dola za kimarekani trillion 1.7 kwa mwaka kwa matumizi ya silaha.

Akasema matumizi ya kiasi hicho cha fedha kujilimbikizia silaha katika maghala mbali mbali duniani huku mamilioni ya watu wakiendelea kuishi katika umaskini uliopindukia, na maelfu ya watoto wakiathirika kwa utapia mlo na wengine wakipoteza maisha kwa kukosa chakula na huduma nyingine za msingi ni jambo lisilokubalika.



Post a Comment

0 Comments