Tume inawataka wale wote ambao
hawajachukua shahada zao katika ofisi za Tume za Wilaya kuharakisha kuchukuwa
shahada zao, kwani zoezi la utoaji wa shahada hizo katika afisi za Wilaya
litasitishwa ifikapo tarehe 19/10/2015, na litaendelea kufanyika Makao Makuu ya
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar yaliyopo Maisara kwa upande wa Unguja na ofisi
ndogo ya uchaguzi ya iliyopo Chakechake Pemba hadi litakapotoka tangazo
jengine.
Aidha tume inawaomba wananchi
kuzingatia muda uliotolewa wa uchukuwaji wa shahada za kupigia kura katika
ofisi za Wilaya kwa lengo la kuondoa usumbufu utakaoweza kujitokeza.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inaomba
mashirikiano kwa kulifanikisha zoezi hili.
Piga kura kwa amani upate maendeleo
nchini
Ujumbe huu umeletwa kwenu na tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
0 Comments