MSAIDIZI Katibu Mkuu wa Umoja wa Watu Wenye
Ulamavu Zanzibar ‘UWZ’ kanda ya Pemba, Salim Abdalla, akitofafanuzi wa mafunzo
ya elimu ya uchaguzi, kwa watu wenye ulemavu wa aina tofauti, yaliofanyika
skuli ya sekondari Madungu Chake chake, katikati ni Afisa miradi kutoka
shirikisho la ‘SHIVYAWATA’ Tanzania Isac Kidama na kushoto ni mtoa mada Asha
Aboud, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Miradi kutoka shirikisho la vyama vya watu
wenye ulemavu Tanzania ‘SHIVYAWATA’ Isac Kidama, akielezea namna ya mradi wa
uchaguzi Jumuishi, kwenye mafunzo ya elimu ya uchaguzi yaliowashirikishwa watu
wenye ulemavu, na kufanyika skuli ya sekondari Madungu Chake chake, kulia ni
Msaidizi Katibu Mkuu wa ‘UWZ’ Salim Abdalla na kushoto ni mtoa mada Asha Aboud,
(Picha na Haji Nassor, Pemba).
MSHIRIKI wa mafunzo ya elimu ya uchaguzi,
ambae ni mlemavu wa usikivu, kutoka wilaya ya Chake chake, akifafanua jambo
kwenye mafunzo hayo, yaliofanyika skuli ya sekondari Madungu Chake chake,
yaliotayarishwa na shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania
SHIVYAWATA, (Picha na Haji Nassor,
Pemba)
WASHIRIKI wa mafunzo ya elimu ya uchaguzi
ambao ni watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali kisiwani Pemba, wakimsikiliza
mtoa mada hayupo pichani, mafunzo hayo yamefanyika skuli ya sekondari Madungu
Chake chake Pemba, (Picha na Haji
Nassor, Pemba).
0 Comments