Baadhi ya makaburi yaliopo Mwanakwerekwe hii ni sehemu muhimu ya kukumbushana mauti kwani Mtume Swalla Allaahu 'alayhi Wasallam alituusia sana tukumbuke sana kile kinachoondosha na kuvunja ladha akikusudia mauti.

 Baadhi ya makaburi yaliopo Mwanakwerekwe sehemu ambayo ilianza kutumika kwa kuzikia tokea mwaka 1965 na kwa mujibu wa wasimamizi wa sehemu hii bado ina nafasi ya kutosha kuendelea kuzika maiti zetu.
 Wakati ukiingia sehemu ya makaburi ya Mwanakwerekwe unakutana na ujumbe huu huu muhimu ambao ni dua iliyosuniwa kusomwa wakati wa kufanya ziara makaburini. Kila mwenye kutembelea makaburi iwe ya jamaa zake au ya mtu yeyote ni Sunna kuisoma dua hii. Ipo haja kwa wasimamizi wa sehemu hii kulifanyia ukarabati bango hili 
 Wakati nilipofanya ziara ya kutembelea makaburi ya Mwanakwerekwe nilikutana na msimamizi mmoja ambae anafanya kazi ya kuchimba makaburi katika sehemu hii tokea mwaka 1995. Msimamizi huyu alinishangaza kwa uzoefu wake kwani kila nikimtaja mmoja wa jamaa zangu na kuulizia wapi lilipo kaburi lako alinipeleka moja kwa moja kaburini hapo bila ya kukosea. Amenipa somo moja kubwa sana kuhusiana na uzoefu wae wa kuweka kumbukumbu kichwani kwa uhakika.
Mlango mkuu wa kuingilia sehemu ya makaburi ya Mwanakwerekwe ambayo ni safari ya mwisho ya kila aliyejaaliwa uhai atapaswa kuikabili.