Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Eng. Patrick Mfugale ambaye alikuwa akielezea hatua za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 linalounganisha kati ya Wilaya ya Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza ambapo limefikia asilimia 27, huku Daraja la kupitisha vifaa likiwa limekamilika kujengwa kwa asilimia 100.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Barabara nchini (Tanroads) Eng. Patrick Mfugale ambaye alikuwa akielezea jinsi
ya kushusha nondo zilizosukwa katika umbo la duara katika mashimo marefu
yaliyochimbwa ndani ya maji ya ziwa Victoria (haonekani pichani)
Nondo zilizosukwa kwa umbo
la duarazikishushwa ndani ya moja ya shimo refu lililochimbwa ndani ya maji ya
ziwa Victoria katika hatua zinazoendelea za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli
lenye urefu wa Kilometa 3.2 Kigongo mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ujenzi wa moja na Nguzo ambayo imeshawekewa
zege katika muendelezo wa kazi za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu
wa Kilometa 3.2 Kigongo mkoani Mwanza.







0 Comments