6/recent/ticker-posts

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akihutubia na kuifungua semina kuhusu Muungano kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari wa Zanzibar, semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Jijini Zanzibar na kuwashirikisha Wahariri na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akihutubia na kuifungua Semina ya Simu moja kwa Wahariri wa vyombo vya Habari Zanzibar na Waandishi kuhusu Muungano, iliyofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Jijini Zanzibar. 
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi, akizungumzav na kutowa maelezo kuhusiana na Semina ya Siku moja kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi kuhusu Muungano iliyofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Jijini Zanzibar. 
Dkt. Harrison Mwakyembe akiwasilisha Mada Muungano: Chimbuko, Msingi na Fursa za Muungano wakati wa Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar kuhusiana na Muungano iliyofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Jijini Zanzibar.
Viongozi wa meza kuu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akifuatilia Mada kuhusi Chimbuki,Msingi na Fursa za Muungano ikiwasilishwa na Dkt.Harrison Mwakyembe, katika semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa ZURA Maisara Jijini Zanzibar na (kulia kwake) Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera,Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe.Hamza Hassan Juma na (kushoto kwake) Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari Zanzibar na Waandishi wa habari wakifuatilia Mada ikiwasilishwa na Dkt.Harrison Mwakyembe ya Chimbuko,Msingi na Fursa za Muungano, wakati wa Semina ya Siku moja kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa jengo la ZURU Maisara Jijini Zanzibar.
























 

Post a Comment

0 Comments