Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Tume kilichofanyika tarehe 2 Februari, 2026, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria kuhakikisha mchakato mzima wa uchaguzi unakamilika kwa uwazi, ufanisi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo Kwa mujibu wa ZEC,
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari makao makuu ya ZEC Maisara,Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe.Jaji George J. Kazi alisema zoezi hilo linafanyika kwa kuzingatia kifungu cha 98(3) cha Sheria ya Uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018, kinachoitaka Tume kuharibu nyaraka zote zinazohusiana na Uchaguzi Mkuu baada ya kupita siku 90 tangu kukamilika kwa uchaguzi husika.
Mwenyekiti ameeleza kuwa kabla ya kuidhinisha utekelezaji wa zoezi hilo, ilijiridhisha kuwa hakuna amri yoyote ya Mahakama inayozuia utekelezaji wa hatua hiyo, hali iliyoiwezesha kutekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa sheria baada ya kukamilika kwa muda uliopangwa
Aidha, amewahimiza wadau wote wa Uchaguzi kushirikiana ipasavyo katika utekelezaji wa zoezi hilo ili kuhakikisha linafanyika kwa mafanikio, uwazi na kwa kuzingatia kikamilifu misingi ya kisheria na taratibu zilizowekwa.

0 Comments