6/recent/ticker-posts

Zoezi la utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Czech-Tanzania Development Chamber of Commerce (CTDCC)

 


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Mhe. Badria Atai Masoud, leo ameshuhudia zoezi la utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Czech-Tanzania Development Chamber of Commerce (CTDCC), kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed.
Makubaliano hayo yanaweka msingi wa ushirikiano wa muda mrefu wa miaka mitano katika maeneo ya maendeleo ya reli, usafiri wa anga, bandari pamoja na miundombinu mingine ya kimkakati, kwa lengo la kuimarisha uchumi wa Zanzibar, kuvutia uwekezaji na kuleta teknolojia za kisasa katika sekta ya miundombinu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Badriya amesema ushirikiano huo unatarajiwa kuongeza ufanisi wa miundombinu ya nchi, kujenga uwezo wa wataalamu wa ndani kupitia mafunzo na ubadilishanaji wa uzoefu, pamoja na kufungua fursa zaidi za ajira kwa vijana.
Ameongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo kwa uwazi na weledi, kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inaleta tija kwa wananchi na kuzingatia kikamilifu maslahi ya taifa.

Post a Comment

0 Comments