6/recent/ticker-posts

KAIMU WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

Na Maelezo Zanzibar   13.03.2026

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetenga zaidi ya Bilioni 4 kwa ajili ya upandaji miti katika maeneo yenye mmong’onyoko wa ardhi ambayo yameathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika nukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuhusiana na siku 100 za mafanikio ya uongozi wa DK. Mwinyi, Kaimu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Hamza Hassan Juma amesema Serikali itashirikiana na wananchi katika kupanda miti ili kurejesha mazingira katika maeneo yaliyoathirika na mmong’onyoko wa ardhi.

Aidha amesema Shilingi Bilioni 1 zimetegwa kwa ajili ya program ya urithi wa Zanzibar ya Kijani (Green legacy) ambapo Serikali itatoa miche ili kuzuia uharibifu wa mazingira.

Amesema Serikali imefanya utafiti wa maeneo yaliyoathirika na mabadiliko ya tabianchi ambapo jumla ya maeneo 62 ya Pemba yamefanyiwa tafiti hizo, miongoni mwa taarifa zilizokusanywa ni pamoja na taarifa za ukubwa wa maeneo, athari ziliopo na kutaarisha ramani.

Kwa upande wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Serikali imeanzisha kituo maalum cha kupokea taarifa kutoka kwa wananchi kupitia namba bure 119 amnbapo jumla ya taarifa 350 zimepokelewa na kumewezesha kukamatwa kwa wahalifu na nyingine zinaendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi.

“Mamlaka imegundua na kusambaratisha mitandao miwili mikubwa ya biashara ya dawa za kulevya pamoja na kutaifisha mali za wahalifu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 169 pamoja na nyumba nne” ameeleza Kaimu Waziri.

Amefahamisha kuwa Serikali pia imeendelea kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu kwa kuwawezesha kupata mikopo kupitia Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (ZEEA), ambapo watu 32 kati ya 34 waliounganishwa wamepatiwa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 82 kwa ajili ya kujiajiri.

Amefafanua kuwa Serikali inachukua hatua madhubuti katika kukabiliana na changamoto za upungufu wa rasilimali fedha ambazo huathiri upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vya UKIMWI kwa kuimarisha mifumo ya ndani ya fedha, kuongeza ubunifu na mashirikiano na wadau katika utafutaji wa rasilimali hizo pamoja na kuhakikisha fedha zinatumika kwa ufanisi na uwajibikaji.

Post a Comment

0 Comments