Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakiwa katika ziara ya kukagua ya ujenzi wa mferejei wa skimu ya umwagiliaji ya Ipwasi Ndorobo katika kijiji cha Kipera kupitia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya Iringa leo Machi 12, 2026. Mbele ni Mratibu wa Mradi huo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Damas Mapunda.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa wameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange na watendaji wa ofisi hiyo walitembelea Mfereji wa Skimu ya umwagilia yenye urefu wa mita 3,500 una thamani shilingi milioni 86 na ujenzi wa jengo la kiwanda kidogo cha kuchakata mahindi wenye thamani ya shilingi milioni 116.6.
Akizungumza wakati wa kutembelea miradi hiyo, Mhe. Kiswaga alisema kamati imeridhishwa na utekelezaji wake na kuwa inaleta manufaa kwa wananchi kwa kuwaingizia kipato kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Halikadhalika, Mhe. Kiswaga ambaye pia ni Mbunge wa Kalenga aliwaomba wananchi waendelee kuitunza miradi inayotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuiendeleza ili iendelee kuwanufaisha.
Kwa upande wake, Dkt. Dugange alisema Ofisi hiyo inatekeleza miradi ya mazingira ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli mbadala zizikuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.
Alisema pamoja na mradi huo wananchi wanapaswa kuendelea kupanda miti na kuitunza ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo yanasababisha mafuriko, ukame na maradhi.
Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Kituo cha Taifa cha Uratibu wa Kaboni (NCMC) itaendelea kuyafikia maeneo mbalimbali nchini ambayo yana misitu kuona namna ya kutekeleza wa miradi hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wakipata maelezo katika ziara ya kukagua kituo kukusanyia maziwa katika kijiji cha Ilalasimba, Kata ya Nzihi kutokana na Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya Iringa Machi 12, 2026.
Mwenyejkiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akizungumza mara baada ya kamati hiyo kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Iringa leo Machi 12, 2026 kabla ya kuanza ziara ya kukagua Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR-Tanzania) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais. Kishoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James.

.jpg)
0 Comments