6/recent/ticker-posts

TAMKO YA SERIKALI SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI 24MACHI 2026


 DODOMA:TAREHE 24 MACHI, 2026

Tanzania inaungana na Nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu
Duniani. Siku hii hutengwa kwa ajili ya kuongeza jitihada na mikakati ya kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu ifikapo Mwaka 2030.

Aidha, siku hii hutumika kutoa hamasa na elimu kwa jamii juu ya uwepo wa ugonjwa huu na njia za kujikinga. Kwa mwaka wa 2026, kauli mbiu ya siku ya Kifua Kikuu Duniani, inasema, “Kwa Jitihada za Pamoja za Viongozi, Wadau na Wananchi, inawezekana Kutokomeza Kifua Kikuu nchini”. Kauli mbiu hii imejikita katika kukumbusha na kuhamasisha viongozi, wadau na wananchi wote juu ya wajibu tulionao katika kuchochea jitihada za kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini.

Ugonjwa wa Kifua Kikuu unasalia kuwa miongoni mwa magonjwa hatari zaidi ya
kuambukiza duniani licha ya uwepo wa matibabu. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika
la Afya Duniani (WHO) ya Mwaka 2024, Tanzania imepiga hatua kubwa katika
kupunguza maambukizi mapya ya ugonjwa huu.

Mathalani, visa vipya vimepungua kutoka wagonjwa 306 kwa kila watu 100,000 mnamo 2015 hadi 172 kwa kila watu 100,000 kwa mwaka 2024 sawa na punguzo la asilimia 44. Aidha, vifo vitokanavyo na ugonjwa vimepungua kutoka 56,000 mwaka 2015 hadi vifo 23,500 mwaka 2024sawa na punguzo la asilimia 59. Kiwango hiki kimepelekea Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache duniani zilizo katika hatua nzuri ya kufikia lengo la dunia la kutokomeza ugonjwa huu ifikapo 2030.

Mafanikio haya, yanatokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika kuboresha
miundombinu ya kutolea huduma hasa kwenye kuongeza mtandao wa uchunguzi na
upimaji kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Aidha, upatikanaji wa dawa za kutibu ugonjwa pamoja na kuhakikisha wagonjwa waliogundulika wanatumia dawa mpaka mwisho ili kudhibiti usugu wa vimelea vya Kifua Kikuu kwa dawa zinazotumika.

Aidha, pamoja na mafanikio haya, Serikali inaendelea kuwekeza katika kutoa huduma bora, zinazoendana na matarajio, ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma hizi Jirani na mwananchi. Aidha, katika kuungana na ulimwengu Wizara ya Afya imeendelea kutoa hamasa ya uelewa wa ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa kutumia njia mbalimbali za
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA
TAMKO LA MGANGA MKUU WA SERIKALI SIKU YA KIFUA KIKUU
DUNIANI2
vyombo vya Habari, elimu ya afya kwa kutumia watoa huduma za afya na wahudumu ngazi ya jamii.

Katika kuhakikisha mafanikio haya yanafikiwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Afya na Sekta zote inaendelea kutoa wito
kwa jamii nzima kuchukua hatua mbalimbali ili kupunguza mnyororo wa maambukizi mapya katika jamii zikiwemo;-

1. Kujitokeza kupima mapema kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa mtu
yeyote mwenye dalili kama za kukohoa, homa za mara kwa mara, kutoka jasho
la usiku au kupungua uzito.

2. Kwa wagonjwa na jamii kuhakikisha mgonjwa aliyeanza matibabu, anazingatia
matibabu kwa ukamilifu kama inavyoelekezwa na wataalam wa afya na
kuhakikisha wanakamilsha dozi ili kuepuka usugu wa dawa kwa vimelea vya
Kifua Kikuu.

3. Kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu na badala
yake kutoa msaada wa kijamii na kisaikolojia kwani mgonjwa wa Kifua Kikuu
akianza matibabu, hupunguza uwezekano wa kuambukiza.

4. Kuendelea kuchukua tahadhari za kupunguza na kuzuia maambukizi kwa
kuepuka misongamano kwenye vyombo vya usafiri, nyumba na maeneo ya
kazi kwa kuhakikisha kunakuwa na hewa ya kutosha na kuzingatia usafi wa
mazingira.

5. Kuendelea kutoa taarifa kwa wakati iwapo kuna mtu mwenye dalili za ugonjwa
wa Kifua Kikuu ili aweze kufikiwa na kupata huduma za uchunguzi na upimaji.
Aidha, kwa wagonjwa wanaoishi na Watoto na watu wengine, kuhakikisha
wanachunguzwa ugonjwa wa Kifua Kikuu na kupata huduma sahihi kutoka
kwa watoa huduma wa ngazi zote kuanzia kwenye jamii hadi kituo cha kutolea
huduma za afya.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasisitiza umuhimu wa ushirikiano wa jamii katika
kutokomeza Kifua Kikuu, Tuchukue hatua sasa kwa ajili ya afya zetu na za vizazi
vijavyo. Kwa pamoja tunaweza kutokomeza Kifua Kikuu.
Dkt. Grace E. Magembe
 MGANGA MKUU WA SERIK

Post a Comment

0 Comments