Zanzibar Heroes imerudisha kipigo ilichopigwa na Kili Stars walichopigwa katika mchezo wa makundi baada ya kuwafunga ndugu zao kwa goli moja kwa nunge katika mchezo wa kugombea mshindi wa tatu wa Cecafa uliomalizika mchana wa leo Jumapili.
Goli lililomuumiza Maximo pamoja na wachezaji wake lilifungwa na Abdi Sadalla katika dakika ya sabiini ya mchezo.
Ingawa Kili boys walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha ila vijana wetu wa Zanzibar Heroes walikuwa imara kwenye safu ya ulinzi ikliongozwa na Nadir Haroub “Canavaro” na kutorushusu hatari zozote kupenya kutoka kwa washambuliaji wa Kili Stars.
Tunawapongeza vijana wetu kwa kuwa timu ya tatu bora katika medani ya Soka ya Afrika Mashariki na kati na tunatumai zawadi waliyoipata ya Dola 10,000.00 itagawiwa miongoni mwa wachezaji kama ni motisha ya kucheza na kuthamini utaifa wao na nchi yao licha ya mazingira magumu waliyoyakabili katika kushiriki michuano ya Chalenji.

No comments:
Post a Comment