Habari za Punde

KORTINI KWA KUHARIBU MALI YA MTU

Na Mwanajuma Said

KOSA la uharibifu wa mali yenye thamani ya shilingi 50,000 limemfikisha mahakamani kijana mmoja wa miaka 20 mkaazi wa Mwera Wilaya ya Magharib Unguja, kujibu tuhuma hizo.

Mtuhumiwa huyo, Ibrahim Abdalla, alifikishwa mahakamani mbele ya Hakimu wa Wilaya Hussein Makame na kusomewa shitaka hilo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Said Mbwana, dai ambalo alilikana.

Katika madai hayo aliyoyakana mtuhumiwa huyo yalidaiwa kutokea huko Mwera Wilaya ya Magharib Unguja, majia ya saa 5:00 mchana, April 4 mwaka huu.

Hati hiyo ya mashitaka ilifahamisha kuwa mtuhumiwa alivunja ukuta wa nyumba wa matofali wa Hazina Ali na kusababisha hasara ya shilingi 50,000.

Mtuhumiwa alipotakiwa kujibu tuhuma hizo alizikana na kuiomba mahakama impatie dhamana ombi ambalo halikuwa na pingamizi mahakamani hapo.

Hakimu Hussein alimtaka mtuhumiwa kujidhamini mwenyewe kwa bondi ya shilingi 200,000 na wadhamini wawili ambao watasaini kima cha fedha kama hicho.

Pamoja na mtuhumiwa kutekeleza masharti hayo Hakimu Hussein aliiahirisha kesi hiyo hadi April 11 mwaka huu kwa kutajwa tena.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.