Habari za Punde

DK SHEIN AWASILI NYUMBANI AKITOKEA UINGEREZA

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Kamishna wa Polisi Zanzibar wakati alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar - Aman Abeid  Karume.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa pili w Rais Balozi Iddi Seif alipowasili akitokea ziarani Uingereza.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein  akisalimiana na viongozi wa vyama na serikali alipowasili katika uwanja wa ndege Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akivishwa shada la mauwa na mtoto Hafsa alipowasili ktika Uwanja wa ndege wa Zanzibar akitokea ziarani Uingereza

Picha na Ramadhan Othman Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, amerejea nchini leo akitokea Uingereza kwa safari maalum.

Katika safari hiyo Dk. Shein alifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na baadhi ya Maafisa wa serikali.

Katika Uwanja wa ndege wa Zanzibar, Dk. Shein alipokewa na viongozi mbali mbali wa vyama na serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Idd

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.