Na AsyaHassan
OFISI yaMufti wa Zanzibar kwa kushirikiana na kikundi cha vijana wa usafishaji Misikiti(AL-ISLAM MOSQUES CLEANING GROUP) kinatarajia kuzindua rasmi shughuli zausafishaji misikiti katika Wilaya ya Mjini.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Soraga kwawaandishi wa habari, ofisi yake imeamua kuwakusanya vijana waliojitolea kufanya usafi katika nyumba hizo za Mwenyezi Mungu.
Aidha,alisema Ofisi hiyo imefikia uamuzi wa kuanzisha kikundi hicho baada ya uchunguzi uliofanywa kubaini kwambamisikiti mingi na hasa sehemu ya vyoo kuonekana vichafu na kuhitaji kusafishwa.
Soragaalisema uzinduzi wa kazi hiyo unategemewa kufanyika leo asubuhi katika msikitiMkuu wa Mwembe Shauri ambapo mgeni rasmianatarajiwa kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji Khamis.
Alifahamishakuwa wakati shughili hiyo ikizinduliwa misikiti ya Gongoni,Nambari,Mabati,Mkutina msikiti wa Sheikh Nassor Bachu wa Kikwajuni tayari imeshafanyiwa usafi nakikundi hicho.
AidhaKatibu wa Mufti alitoa wito kwa waumini mbali mbali kukiunga mkono kikundihicho kwa kusaidia kuchangia vifaa mbali mbali vya usafishaji ili kufanikisha shughuli hiyo muhimu.
No comments:
Post a Comment