Habari za Punde

ZANZIBAR YAIOMBA ISRAEL KUISAIDIA NISHATI MBADALA

Na Abdulla Ali, OMPR

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameiomba Serikali ya Israil kuangalia uwezekanao wa kuisaida Zanzibar katika upatikanaji Nishati mbadala ya umeme kwa lengo la kuepukana na kutegemea chanzo cha  aina moja pekee.


Balozi Seif aliyasema hayo katika mazungumzo yake na Balozi wa Israil Kanda ya Afrika Mashariki anayeishi Nairobi, Jacob Keldar, aliyefika kumuaga baada ya kumaliza muda wake.

Makamu wa Rais alieleza kuwa Zanzibar inategemea aina moja tu ya upatikanaji wa nishati hyo muhimu kwa maendeleo ya nchi, jambo ambalo linaweza kusababisha hasara kubwa iwapo chanzo hicho kitafeli na kukosekana mbadala wake.

Aliiomba nchi hiyo kutumia utaalamu wake na kuangalia uwezekanao wa kuanzisha mitambo ya kuzalisha umeme wa upepo, jua au vianzio vyengine.

Halikadhalika, aliomba misaada ya kusaidia sekta nyengine kama maabara ya Mifugo, taaluma ya ufugaji kuku kibiashara, ufugaji wa samaki na mafunzo kwa madaktari wa Zanzibar, pamoja na kilimo cha umwagiliaji kwa matone.

Naye Balozi wa Israil anayemaliza muda wake, Jacob Keldear alisema wawekezaji na makampuni mengi nchini kwao wamevutiwa na Zanzibar na kuonesha nia ya kutaka kuwekeza hapa nchini ikiwemo kampuni ya utengenezaji meli.

Alisema tayari ameshakutana na baadhi ya viongozi wa sekta mbali mbali kama Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Waziri wa Mifugo na anatarajia kukutana na Waziri wa Habari, Utamaduni,   Utalii na Michezo kuzungumzia masuala ya maendeleo na uwekezaji.

Aidha alieleza kufurahishwa kwake na hali ya usalama na utulivu uliopo nchini na kusema ni moja ya kivutio muhimu kinachowafanya wafanyabiashara na wawekezaji wengi kuvutika kuwekeza

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.