Habari za Punde

DK SHEIN AFARIJI MAJERUHI WA MELI ILIYOZAMA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akimfariji Sharif Juma Sharif, kutoka Maziwa Ngombe kisiwani Pemba akiwa ni katika majeruhi katika ajali ya meli ya Spice Islander, iliyozama katika bahari ya Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) Makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Mama Mwanamwema Shein, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,Pembe Juma wakiwa katika hali ya majonzi walipofika katika kijiji cha Nungwi kuangalia hali halisi ya matukio ya majeruhi katika Meli iliyozama ya Spice Islander.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi walionusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja jana
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha jeshi la polisi (FFU) pamoja na wnaharakati wengine wa uokozi wakibeba majeruhi aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja jana.
Baadhi ya wanajeshi wa vikosi mbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi Marium Mohamed Muradi (29) kutoka Tanga,aliyenusurika na kifo katika ajali ya kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika ufukwe wa bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akiwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja.

skari wa vikosi nbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi waliookolewa katika meli iliyozama huko katika Bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja,wakifikishwa katika ufukwe wa Nungwi.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja,Nasra Muhsin,wa Ole Pemba akiwa amelazwa katika hopitali ya Kivunge kaskazini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akifutana na msaidizi mkuu wa Kituo cha Afya kivunge,Tamim Hamadi, baada ya kuwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander, Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja.

Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.