Habari za Punde

CHAMA CHA WAKULIMA CHASHAURI NJIA MPYA ZA KIUCHUMI

Na Hadia Khamis

MKURUGENZI, Mipango na Uendeshaji sera wa chama cha Wakulima ameiomba serikali ijikite zaidi na masuala ya ndani ya nchi ili kukuza uchumi wake na kuinua hali ya maisha ya wananchi kwa kuzingatia nchi
wingi wa rasilimali ziliopo nchini.

Hayo aliyasema Mkurugenzi wa mawasiliano wa chama hicho Rashid Mchenga wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake, Kikwajuni.


Aidha alisema pamoja na viongozi wengi wa serikali kwenda nje kutafuta misaada basi jukumu kubwa ni kuwepo ufuatiliaji wa ahadi zinazofikiwa na viongozi hao.

Hata hivyo, alisema kuwa chama cha wakulima imeishauri serikali kupitia serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuvitumia vikosi vyake vya kiuchumi kuinua uchumi wake hasa kwa kuanzisha mazao mbadala, kupanda
pamoja na kulima mazao kama vile vanila, hiliki , pilipili hoho na mlangi langi, mazao ambayo yanabei kubwa katika soko la dunia hivi sasa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.