Kamati ya maadili yamuhoji kwa saa kadhaa
Asema kutangaza nia ni haki yake kikatiba
Na Kunze Mswanyama, Dar
CHAMA cha CUF, huenda kikaiga hatua za chama cha NCCR Mageuzi kilichomtimua Mbunge Kasulu David Kafulila, nacho kwa kumuonesha njia ya kutokea ndani ya chama hicho Mbunge wa Wawi Chake Chake Pemba, Hamad Rashid Mohammed.
Hatua hiyo inafuatia baada ya jana kamati ya maadili ya CUF, kumuweka kikaangoni Mbunge huyo pamoja na wanachama wengine wanane waandamizi wanaomuunga mkono kwa kile kinachodaiwa kuwa ni uasi.
Mbunge huyo na wanachama hao wakiwemo baadhi yao wajumbe wa Baraza Kuu, walipigishwa magoti chini ya kamati ya maadili ya CUF, baada ya kubainika kuwa ni vinara na chanzo cha migogoro.
Awali kabla ya kamati hiyo kuwaita Hamad Rashid na kundi lake lililoibua uasi ndani ya chama, kamati hiyo ilipitia tuhuma za wanachama hao na kubaini wana tuhuma za kujibu ambapo waliandikiwa barua zilizowataka wafike mbele ya kamati hiyo.
Kamati ya Maadili ya CUF, iliketi jana Makao Makuu ya chama hicho hicho yaliopo Buguruni jijini Dar es Salaam, huku ulinzi mkali ukiimarishwa nje ya ofisi hizo na kuzuiwa yeyote asiyehusika kupata habari yoyote ya kile kinachoondelea kujadiwa kwenye kamati hiyo.
Baada ya kuhojiwa, Mbunge huyo aliyewahi kuiongoza kambi ya upinzani katika Bunge la tisa, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, kutangaza nia juu ya kuwania nafasi yoyote ndani ya chama ni fursa iliyopo
kikatiba.
Mgogoro ulianza baada ya Mbunge huyo kutangaza rasmi kuanza harakati za kutaka kugombea nafasi ya Ukatibu Mkuu inayoshikiliwa na Maalim Seif Sharif Hamad ambaye kwa sasa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Siku chache baada ya Rashid kutangaza kuwania kiti hicho, Naibu Katibu Mkuu Bara, Julias Mtatiro aliwaambia waandsihi wa habari kuwa, kilichofanywa na mbunge huyo ni sawa na uasi jambo lililomfanya Rashid kutaka ajulishwe uasi wake ni upi.
Hata hivyo badala ya kujibu hoja yake,walianza kumtuhumu kuwa anajaribu kuandaa mapinduzi jambo lililowafanya baadhi ya viongozi waandamizi kuanza ziara za mikoani kuwaambia wanachama kuwa huyo ni
muasi ambapo kikosi cha ulinzi cha chama hicho kinachojulikana ‘Blue Guard’ kilianza kuvamia mikutano yoyote inayohudhuriwa na mbunge huyo.
Baadhi ya wachunguzi wa mambo ya kisiasa,wamesema kuwa kuna kila dalili za kuanza kutoamika kwa baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani kufuatia chama cha NCCR Mageuzi kumtimua Mbunge wa Kasulu Mjini, David Kafulila kwa kile kilichosemwa kuwa ni uasi ndani ya chama.
Hata hivyo, ukweli ni kuwa demokrasia ndani ya vyama hivyo imefinywa jambo linalowafanya wale viongozi waandamizi kuanza kupatwa na kiwewwe wakidhani kuwa watapokonywa madaraka yao na vijana ambao wanakuja kwa kasi zaidi.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na vyombo vya habari walisema kuwa kama Hamad Rashid amekichoka chama ahame kwa salama na sio kuzusha chokochoko.
“Chama ni cha wanachama na sio cha mtu fulani, anayejihisi amachoka aondoke, wapo watu wengi ndani ya chama wanaweza kuongoza”, alisema mmoja kati ya wafuasi wa chama hicho.
Walisema kuwa mgogoro huo ukiendelezwa unaweza kuviza shughuli nyingi zenye maslahi ya taifa hasa suala la utoaji wa maoni katika mpya ambalo linatarajiwa kuaza hivi karibuni.
Salamu zangu kutoka Ufaransa! Baada ya kutembelea blog yako, sikuweza kuondoka bila kuweka maoni.
ReplyDeleteNawapongeza kwenye blog yako!
Labda ningekuwa na nafasi ya kuwakaribisha kwenye mgodi pia!
siku njema
cordially
Chris
http://sweetmelody87.blogspot.com/