Habari za Punde

WARSHA YA KURIPOTI HABARI ZA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO KWA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR ILIOANDALIWA NA TAMWA NA UNFPA.

 Mkuu wa Dawati la Wanawake na Watoto katika Kituo cha Polisi Madema Fakhi Yussuf, akiwasilisha mada ya Kesi za Udhalilishaji wa Watoto na Wanawake zinazoripotia katika Dawati hilo na kuchukulia hatua za Kisheria.katika warsha ya waandishi wa habari kuripoti habari za Udhalilishaji Kijinsia Zanzibar.ilioandaliwa na UNFPA na TAMWA.   
 Mkuu wa Dawati la Wanawake na Watoto Fakhi Yussuf, akisisitiza jambo, katika Warsha ya waandishi wa habari kuripoti  habari za Udhalilishaji Kijinsia, iliofanyika Ukumbi wa Jengo la Baraza la Habari Mlandege Zanzibar.   
Wanaharakati wa kupambana na Udhalilishaji wa Kijinsia wa Watoto wakimsikiliza mtowa mada Fakhi Yussuf akiwasilisha mada yake. 
 Wanahabari wakiwa makini kusikiliza Mada mbalimbali zilizotolewa katika Warsha ya kuripoti habari za Udhalilishaji Zanzibar.
 Mwanaharakati kutoka  TAMWA, Mzuri Issa, akiwasilisha mada ya Umuhimu kwa Vyombo vya Habari kupambana na Ukatili wa Kijinsia, wanaofanyiwa Watoto na Wanawake, jinsi ya kuripoti na kuielimisha Jamii kutokana na maswala hayo kupitia vyombo vyao.  
 Washiriki wakimsikiliza Mtowa mada, katika Warsha ya Waandishi wa Habari na Wanaharakati   
Mwanaharakati kutoka Kitengo cha Sheria Zanzibar Jamila Mahmuod,akichangia Mada ya Udhalilishaji amesema bado Jamii haijakubali kuhusu tatizo la Unyanyasaji na kushindwa kujitokeza kutowa ushahidi wakati wa tatizo linapotokea, na kesi kumalizika bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha kwa sababu ya Wananchi hawajitokeza kutowa ushahidi.Amesema kuna baadhi ya Wananchi hufuta kesi na kukubali kulimaliza Nyumbani, ndio sababu tatizo hilo linazidi kukuwa kutona  na kila likitokea humalizwa kienyeji.     
 Mwanahabari wa Gazeti la Mwananchi Talib. Ussi, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuunda Dawati la Wanawake na Watoto. Amesema itumike hizi siku kuminasita kutowa Elimu kwa Wananchi kupita Vijiji kwaelimisha kuhusiana na Tatizo hili,amesema wananchi washirikiane mtu mmoja mmoja ili kutowa habari kwa mwengine kupiga vita Ukatili wa Kijinsia Zanzibar.    
 Mwanaharakati kutoka Kitengo cha One Stop Center katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Bi. Fatma , amesema kuwe na ushirikiano na Jeshi la Polisi katika kupambana na Ukatili wa Kijinsia kwa Watoto, kutokana na kesi za Udhalilishaji wanaofanyiwa watoto.Amesema kwa wastani hupata kesi tano kwa siku na kuzifanyia uchunguzi na kama itadhibitika kuwa mtoto ameharibiwa hukabidhi kwa polisi kwa hatua za kisheria, amewataka Wananchi kuwafikisha Watoto katika kitengo hicho kufanyiwa uchunguzi, kwa maana ikipita masaa 24, ushahidi haupatikani. Amewataka waandishi kuielimisha Jamii kuhusu maswala ya Udhalilishaji.   

Mwanaharakati kutoka Makunduchi Zaharani Ame, amesema vitendo vya Ukatili wa Kijinsia viko vingi katika maeneo mbalimbali ya mjini wa Zanzibar na yeye ameshawahi kuripoti kesi za kudhalilishwa kwa watoto sehemu husika na atazidi kufutalia na kupiga vita maswali hayo kwa kadiri ya uwezo wake ili kutokomeza swala hilo kwa jamii.  
Mwanaharakati Asha Iddi Muhidin,kutoka Mfenesini Unguja.Amesema yeye yamemkuta matatizo ya Ukatili wa Kijinsia, kwa Mwanawe ambaye amekuwa akipata kipigo na hatimai kuharibu mimba mbili na kupoteza kizazi kutokana na kipigo alichokuwa akipiwa na huku akiwa na mimba, Na yeye alipata udhalilishaji kutoka kwa jamaa wa Mkewe walipigwa mpaka akapoteza fahamu kwa siku tatu, lakini mpaka sasa hakuna hatuwa ilioochukuliwa na anazidi kuhangaika yeye na mumuwe ili kupata haki ya msaada wa kisheria. kupitia kitengo cha Wanasheria Wanawake Zanzibar. (ZAFELA ) 
Mwanahabari Issa Yussuf, amewataka Wananchi wabadiliki katika matatizi ya Udhalilishaji, wakati linapotokea kila mtu anashindwa kutowa ushirikiano wa jombo hilo, katika kutowa ushahidi katika vyombo husika.Inabidi waandishi tutumia kalamu yetu kuielimisha jamii kupiga vita Udhalilishaji wa Kijinsia,ndio tutaweza kupunguza tatizo hili katika jamii.   
Mwanaharakati kutoka Kiboje Wilaya ya Kati Unguja Jaribu Mwinyi Khamis,amewata akinamama kuwacha kuwadekeza watoto wao wa kike ndio chanzo cha matatizo ya kupata Ukatili ya Kijinsi, pale Akinababa wanapowagomba wao huwa mbele kwaombelezea. na hatimai hutokea tayizo la kutoroshwa au kubakwa.Amesema inafikia mtoto wa kike hudiriki kutowa utovu wa adabu kwa mzazi wake.Amewtaka wakinamama kuwaelimisha watoto wao. 
 Mwanaharakati wa Ukatili wa Jinsia Jina Mwinyi Waziri. Amesema jamii haitaki kubadilika katika Jambo hili,asilimia kubwa ya Ubakaji humalizika katika mikono ya Polisi kwa makubaliano ya kuoana au kilipa fidia kwa mtendewa,bila ya kufikishwa katika sehemu hisika za kisheria na kupata maamuzi ya kisheria.ndio maana kila siku jambo hili huzidi kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji. 
 Mwanaharakati kutoka Kaskazini Unguja Mwanajuma Kassim, amesema watoto wanafikia hatuwa ya kubakwa kutokana na tamaa walionayo, na kuna baadhi wanasema hujishtukia tayari wameshafanya kitendo hicho bila ya kujijua na kudai kufanyika kwa njia za kiswahili,(ndumba)Amesema amefanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, katika utafiti wake amegunduwa kuna baadhi ya vituo vya polisi wanaporipotiwa matatizo ya udhalilishaji huandika jina moja tu, la mfanyiwa na jina na mfanyaji linakuwa hakuna ndio maana utakuta kesi zikienda mahakamani hukosa ushahidi wa kutosha na mtuhumiwa kuachiwa.amewataka waandisjhi kufuatilia kesi za ukatili wa kijinsia siyo kuziacha baada ya kufikishwa mahakamani kuripoti mara moja halafu basi wananchi hawajui nini kimetendeka.     
Mwanaharakati Sharifa Maulid, akisisitiza jambo wakati akichangia mada ya Udhalilishaji Kijinsia Watoto na Wanawake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.