Timu ya Jamhuri yenye makaazi yake wete Pemba juzi iliyaaga mashindano ya shirikisho baada ya kufungwa mabao 4-1 na timu ya Hwange ya Zimbabwe katika mechi iliyofanyika katika uwanja wa Colliery
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Gombani Pemba wiki mbili zilizopita Jamuhuri ililala 3-0 na hivyo kutolewa kwa jumla ya 7-1
Mabao ya Hwange yalifungwa katika dakika za 25, 45, 47 na 73.
Kocha Mkuu wa Timu ya Jamhuri alilalamika uzoefu wa michezo ya kimataifa ndiyo uliyowaathiri sana na pia kubadilishwa kwa uwanja wa mechi kutoka Harare kwenda Victoria Falls. Kwani Jamhuri ilibidi kusafiri masafa ya kilometa 800 kwa basi na walipofika Victoria Falls tayari walikuwa wamechoka na kupata nafasi ya kufanya mazoezi kwa siku moja tu kabla ya mechi. Uchovu nao kwa kiasi kikubwa ulichangia matokeo
Timu zilikuwa kama ifuatavyo
Hwange: P Mhari, T Sibelo, M Mungadze, E Chipeta, D Boriwondo, O Mpofu (O Lungu 75th min), F Vimisayi, R Chinyengetere, F Zvikumbawire (T Mareya 57th min), A Tavariswa, N Siwela
Jamhuri: J Talib, O Mustafa (M Shamban 48th min), M Said, H Said, M Masoud, J Mmanga, B Futo, S Nuhu, A Mmanga, A Ali (A Mussa 61st min), A Othman
No comments:
Post a Comment