Mabingwa wa Kabumbu Zanzibar Timu ya Mafunzo imeyaaga rasmi mashindano ya CAF baada ya kufungwa magoli 3-0 huko Msumbiji walipopambana na Muculmana. Katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Mafunzo ilifungwa magoli 2-0 kwa hivyo imefungwa jumla ya magoli 5-0.
Ingawa timu ya Mafunzo ilipoondoka iliahidi ushindi dhidi ya timu ya Muculmana, timu ilishindwa kukabiliana na kandanda safi lililokuwa likioneshwa na tim ya Msumbiji.
Mabao ya Muculamana yalifungwa na Steliko Ernesto "Telinho" katika dakika ya kwanza ya mchezo na jengine kupachika kabla ya timu kwenda mapumzikoni. Goli la tatu lilifungwa na Reginaldo Fait katika kipindi cha pili.
Kwa matokeo haya timu ya Msumbiji sasa itavaana na Dynamos ya Zimbabwe na hivyo kuhitimisha safari za timu za Zanzibar kwenye michuano ya Caf kwa msimu. Timu ya Jamhuri iliyokuwa ikishiriki katika kombe la shirikisho nayo imetolewa na timu ya Hwange kutoka Zimbabwe kwa jumla ya magoli 7-1.
No comments:
Post a Comment