Habari za Punde

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utandazaji Zanzibar Hassan Mitawi, akifunguwa Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari, katika ukumbi wa Ecrotanal, na kutowa nasaha zake, kwa Waandishi kutumia kalamu zao uzuri bila ya kukiuka uhuru w mtu mwengine. Amewaasa kuandika habari za uchunguzi na kuzifanyia uchunguzi wa kina, amesema mwandishi ni mtu muhimu katika kuelimisha watu kutoka na habari yake anayotowa bila ya kukiuka uhuru wa mtu na maadili yake ya uandishi.    
Mwandishi Mkongwe wa Habari Zanzibar Salim Said Salim, akitowa mada katika Kongamano la Siku ya Uhuru wa Habari huadhimishwa Duniani kuto ifikapo 3 mei.Kongamano hilo limefanyika katika Ukumbi wa Ecrotanal Zanzibar.
Mwenyekiti wa Zanzibar Press Club Suleiman Seif, akitowa ufafanuzi wa mada iliotolewa na Mwandishi Mkongwe Salim Said Salim, katika kongamano la Siku ya Vyombo vya Habari Zanzibar lililofanyika ukumbi wa Ecrotanal.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar akifunguwa kongamano hilo.
Katibu wa Zanzibar Press Club, Suzan Kunambi, akichangia mada kuhusu uvaaji wa Waandishi na jinsi ya kujipanga wakati  wakijitayarisha kufanya mahojiano, kuna baadhi ya waandishi hutumia lugha sizo za kiandishi.    
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Ussi Talib, akichangia mada ya Uhuru wa Vyombo vya habari, akiuliza Zanzibar ilikuwa na Waandishi wengi wakiripoti kaqtika vyombo vya Nje na Zanzibar inasifika kwa lugha kiswahili kilicho safi. lakini sasa hakuna kitu hicho.
Amesema waandishi wanapoalikwa katika shughuli mbali hutengwa katika mambo ya mafao hupewa kidogo ichukuliwa mualiko umetolewa kwa wate, hili ni uzalilishaji  na kusahau kuwa wao ndio wanaotowa  elimu kwa mambo yaliozungumzwa katika semina hiyo. jee huu sio uzalilishaji kwa waandishi kuwaona wao sio kitu baada ya kumaliza mambo yao.
Amesema waandishi wawe na msimamo wanapokuwa katika kazi yao ya kuelimisha jamii, kazi ya uandishi ni kutowa elimu kwa jamii na kuhabarisha.    
Nae Mwaandishi wa kujitegemea Ayuob amesema kuna baadhi ya waandishi wanaojiita waqpevu hutowa dharau kwa waandishi wachanga wanaochipukia katika kada hiyo ya habari, amewaomba kutowa ushirikiano ili kuikuza sekta hii ya habari hapa Zanzibar kwani na wao wametekea hukohuko. 
Mwanajuma Juma akichangia mada kuhusu baadhi ya Watendaji huwadhalilisha waandishi kwa wanaita katika shughuli zao na kuwaweka  kwa muda mwingi na baada ya muda huwaambia  muhusika hayupo na warudi baadae.
Nae mwandishi wa Jucob amesema Zanzibar Press Club iwe na kali  moja kuhusu usimamizi wa uandishi. na kusema kuna ubaguzi wa baadhi ya vyombo vya habari, katika kuripoti babari  
Mratibu wa Baraza la Habari Zanzibar Shifaa, ameishukuru Zanzibar Press Club, kwa kuandaa kongamano hili la kuwakutanisha waandishi  kujadili mambo ya uhuru wa habari. kila mwaka shughuli hizi hufanywa na Baraza la Habari Tanzania.    
Ofisa wa Habari Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Raya Hamad, amewataka waandishi hasa wa kike kuwa makini na mavyazi yao wanayovyaa wakiwa katika kazi yao, kuna baadhi yao huvuaa nguo ambazo hazistahili kuvaliwa wanapokuwa wakienda kuchukuwa habari, hukutana na sosi wao mbalimballi na kila mtu na mtizao wake. amewataka kuvaa nguzo za kawaidi inayostahili kuingia mahali popote na sasa yoyote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.