Habari za Punde

Dk. Shein Akiendelea na Ziara Wilaya ya Kusini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi alipowasili katika Hifadhi ya Taifa ya Jozani, kuangalia ufungaji wa Kasa Jozani. akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili  Afan Othman, akitowa maelezo  ya ramani ya mipaka ya Hifadhi ya Msitu wa Hifadhi wa Taifa , kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipotembelea mradi huo wa Wananchi wa maeneo ya hifadhi ya msitu wa Jozani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Mradi wa Ufugaji Kasa Jozani, Mohammed Salum Haji, akitowa maelezo ya mradi wao wa ufugaji wa Kasa katika hifadhi ya msitu wa Jozani, wakati Rais wa Zanzibar alipotembelea mradi huo na kuona maendeleo yale, unaomiliokiwa na Wananchi  wa Maeneo ya msitu huo. 
Kasa wakiwa katika msitu wa hifadhi ya Jozani.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea daraja la mbao linalozunguka eneo la mikoko katika msitu wa Jozani, likiwa ni moja ya kivutio cha Watalii wanaotembelea msitu huo kuangalia  miti ya mikoko iliokuweko katika eneo lililopita daraja hilo.

Ras wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Afan Othman, akitowa maelezo ya  Bonde la Mpunga la Muyuni kwa Rais wa Zanzibar alipotembelea bonde hilo wakati ziara yake kutembelea shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Mpunga wa Wakulima wa Bonde la Muyuni ukiwa umechanua, kutoka na kupata mbolea na maji ya kutoka katika kipindi hichi cha Mvua za masika zinazoendele.  
Sheha wa Shehia ya Muyuni Mzee Ali, akitowa maelezo yake kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipofanya ziara ya kuwatembelea Wakulima wa Mpunga wa Bonde la Muyuni, kuona mafanikio yao katika Kilimo cha Mpunga, na matatizo wanayokabiliana nayo katika kilimo hicho.  
Mkulima wa Bonde la Muyuni akisoma risala kwa niaba ya wakulima wezake mbele ya Rais wa Zanzibar, alipofika kuwatembelea katika bonde lao huko Muyuni, na kuridhishwa na ukulima wao, katika risala yao wakulima hao wamemuomba rais kuwapatia Treka lao kwa ajili ya Kijiji cha Muyuni na mashine ya kusagia mpunga
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed  Shein, akikata utepe kuashiria kuzinduwa Madarasa mapya ya Skuli ya Mtende Wilaya ya Kusini Unguja yaliofanyiwa ukarabati na jumuiya ya WHY - World Home for Youth, yenye Makao yake Nchi Italia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea moja ya madarasa hayo baada ya  kuyazinduwa, wakati wa ziara yake Mkoa wa Kusini Unguja.
Mjenzi wa Ukarabati wa Madarasa ya Skuli ya Mtende wa Kampuni ya Mchanganyiko Francesco Camerlingo, akitowa shukrani zake kwa Wananchi wa Mtende kwsa Ushirikiano wao katika shughuli za maendeleo ya Kijiji chao.
Mwakilishi wa World Home for Youth Zanzibar Juma Mahmoud, akitowa salamu ya Jumiya yao kwa Rais wa Zanzibar na Wizara ya Elimu kwa ushuirikiano wao mzuri, kufanikisha ujenzi huo wa Skuli ya Mtende.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mtende baada ya kuwazindilia madarasa yao mapya. yaliofanyiwa ukarabati na Jumiya ya World Home for Youth (WHY).
Wazee wa Kijiji cha Mtende wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwahutubia baada ya kuzinduwa madarasa mpya ya skuli ya Mtende, akiwa katika ziara ya  kutembelea Mkoa huo kujionea shughuli za maendeleo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.