Na Salum Vuai, Maelezo
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limemteua Masoud Attai Masoud, kuwa mjumbe wa Kamati Tendaji wa baraza hilo.
Tayari, Attai ameanza kazi rasmi ambapo juzi Julai 14, alikuwa kamisaa katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya Kombe la Kagame kati ya APR ya Rwanda na Wau El Salaam kutoka Sudan.
Attai ambaye kwa miaka mingi amekuwa Katibu msaidizi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ameelezea kuteuliwa huko kuwa ni changamoto ya kuonesha kwamba Wazanzibari wana uwezo wa kusimamia shughuli za soka kitaifa na kimataifa.
"Naishukuru CECAFA kwa kuniona na kuniamini kuwa ninafaa kwa nafasi hii, ninaahidi kufanya shughuli zangu vyema kwa faida ya ZFA na Zanzibar kwa jumla", alieleza Attai.
Kwa mujibu wa barua ya CECAFA iliyotumwa kwa ZFA, uteuzi huo umeanza Julai 10, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment