Habari za Punde

Balozi Seif Akutana na Bodi ya Wakurugenzi Zato na Ujumbe wa Kampuni Inayozalisha Umeme wa Takataka

 Makamu waPili wa  Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Jumuiyaya Makampuni ya Watembeza Watalii Zanzibar { ZATO } baada ya kuzungumza naohapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kulia ya Balozi Seif niMwenyekiti wa Jumuiya ya Watembeza Watalii Zanzibar Bw. Khalifa Makame.
  
Makamu waPili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Kampuniinayosimamia mradi wa umeme unaotokana na Taka taka ya Nchini Ufaransa ya { CITELUM} ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Wa mwanzo kulia ya Balozi niBalozi wa Heshima wa Sechelles Nchini Tanaznia Bibi Maryvonne Pool, KanalMstaafu Bwana Laiza na Mkurugenzi Mkuu wa Cetilum Kanda ya Afrika Bwana PierreDoutreloux.
Kushoto ya Balozi ni uongoziwa Wizara ya Maji,Maendeleo ya Makaazi, Nishati na Ardhi ukiongozwa na WaziriRamadhan Abdulla Shaaban.

Picha na Saleh Masoud Mahmoud
OMPR

Na Othman Khamis Ame

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepongezwa kwa uamuzi wake wa kuandaa mpango mpya wa nadharia ya Utalii kwawote ambao umelenga  kuwa na Wataalamu zaidi watakaosaidia Eneo la Utalii linayotarajiwa kuwa Sekta Kiongozi ya Uchumiwa Zanzibar.

Pongezi hizo zimetolewa na Ujumbe wa Bodi yaWakurugenzi wa Jumuiya ya Makampuni ya Watembeza Watalii Zanzibar { ZATO }ulipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Ujumbe huo ukiongozwa na Mwenyekiti wake Khalifa Makame ulimueleza Balozi Seif kwamba hatua hiyo ya Serikali imeleta faraja kwawashirika wengi wa Sekta hiyo ikiwemo Jumuiya yao.

Wamesema Jumuiya yao imeamuakuweka mikakati zaidi katika kuunga mkono mpango huo wa Serikali kwakushirikisha zaidi Wananchi moja kwa moja katika masuala ambayo ni kivutio kwawageni ambayo yamo ndani ya maeneo yao.

“ Kuna vyakula vya asili kama muhogo, ugari, majimbina hata matunda yenye kuzalisha hapa Zanzibar yanaweza kuandaliwa utaratibu mzuri wa kuuzwa katika maeneo ambayo watalii na wageni hutembelea”. Walisema wajumbe wa jumuiya hiyo.

Wajumbe wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi wa Jumuiya yaMakampuni ya Watembeza Watalii Zanzibar{ ZATO } walisisitiza kwamba mipango hiyo ni moja ya utaratibu unaoweza kumnufaisha moja kwa moja Mwananchi kujiongezea kipato”.

Walisema katika kwenda sambamba na sera ya Serikal iKuu ya Utalii kwa Wote Jumuiya yao inafikiria kufanya shughuli zao za kila siku kwa kutumia kadi katika malipo ili kudhibiti ubadhirifu kwa lengo la kuiongezea mapato zaidi Serikali.

Waliongeza kwamba taratibu zinachukuliwa na Jumuiya yao ya kutegemea kuanzisha Tamasha la Biashara hapa Zanzibar litakalotoa fursa kwa washirika wote wa sekta ya Utalii kutangaza Vitu na bidhaa zao wanazozalisha.

Naye Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarBalozi Seif Ali Iddi aliueleza Ujumbe huo kwamba Zanzibar bado haijafanya Utafiti wa kina wakujua Watalii na wageni nini wanakipenda au kukihitaji zaidi wakati wanapoingiaNchini. 

Balozi Seif alisema tatizo linaloonekana ambalo ni la muda mrefu ni namna ya kujipanga zaidi na kuandaliwa mazingira  mapya ambayo Mtalii anaweza kuvutika nayo.

Alizishauri Taasisi zinazosimamia Sekta ya Utalii kujipanga vizuri katika kuutumia muda wenye upungufu wa uingiaji wa wageni {low Season } uendelee kuwa wa kawaida kwa kuweka vishawishi  vitakavyomfanya Mtalii aendelee kuja Nchini  muda wote.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana na Ujumbe wa Kampuni inayozalisha Umeme kwa kutumia takataka ya nchini Ufaransa { CITELUM } yenye Tawi lake BaraniAfrika.

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni hiyo kanda ya Afrika Bwana Pierre Doutrelouxalimueleza Balozi Seif kwamba mradi wao umelenga zaidi kutoa huduma kwenye Mijimbali mbali samba na usafi wa Mji kutokana na maumbile ya mradi wenyewe.

Bwana Pierre alisema mradi huo hufanikiwa vyema katika maeneo husika baada ya jamii inayouzunguuka kupewa Taaluma ya kina ya namna ya matumizi ya ukusanyaji wataka taka.

Mradi kama huo unaotumia eneo la ukubwa wa Hekta 7 tayari umeanzishwa katika Miji ya Mexico, Brazil na Bukinafaso.

Balozi wa Heshima wa Jamuhuri ya  Seychelles Nchini Tanzania Bibi Marry VonnePool aliyeuongoza Ujumbe huo alisisitiza kwamba upo umuhimu wa kusafisha Miji katika maeneo mbali duniani kwa kutumia mradi wa umeme unaotumia Taka taka.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seifameelezea kuridhika kwake na Mipango ya Kampuni ya Citelum ya kuendeleza Mradihuo ambao ni ukombozi wa utunzaji wa Mazingira katika maeneo ya Mjini.

Balozi Seif aliuomba Ujumbe wa Uongozi wa Kampni hiyo kuendelea kukutana na Watendaji wa Taasisi mbali mbali Nchini ili kuangaliamazingira iwapo mradi kama huo unawezakuwekezwa hapa Nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.