Hii ni hali halisi ya eneo la ndani ya ukumbi maarufu wa mikutano uliopo chachani chake chake Pemba ambao asili yake ukumbi huo ulikuwa jingo la sinema.
Maskiini chachani ! Paa lililokuwa na mvua sasa limekuwa kama chungio la kupenyeza vyote hivyo bila ya kizuizi kutokana na kuchakaa kabisa na kushindwa kutoa huduma kama kawaida yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye alifanya ziara ya ghafla kulikagua jingo la mikutano la chachani chake chake Pemba alikuwa akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Canal Mstaafu Juma Kassim Tindwa jinsi ya kulinusuru jingo hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia kwa nje jingo la ukumbi wa mikutano la chachani chake chake Pemba ambalo liko katika hali mbaya.
Mpiga picha Hassan Issa- OMPR-ZNZ
No comments:
Post a Comment