Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto) akiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam, alipotembelea ofisi hizo na kukutanana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohamed (katikati) wakiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam
Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (kushoto) akiongea na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai,alipotembelea Tume hiyo katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Prof. Ghai amekutana na Wajumbe na kubadilishana nao uzoefu kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba ya Kenya Prof. Yash Pal Ghai (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Casmir Kyuki (kushoto) na Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bw. Joseph Ndunguru katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Tume Dar).
No comments:
Post a Comment