Habari za Punde

Habari Tulizozipata Sasa hivi kupitia katika Msikiti wa Rahaleo baada ya Sala ya Adhuhuri.aleo Breking News

Buriani Shekh Nassor Bachu,

Hapari tulizozipata sasa wakati tukisali sala ya Adhuhuri katika Msikiti wa Rahaleo kupitia Kiongozi wa Msikiti huo ametowa Taarifa ya Kufariki Shekh. Nassor Bachu, kilichotokea leo huko mjini Dar-se-Salaam, Shekh Bachu alikuwa akisumbulia na maradhi kwa  kipindi kirefu sasa.

Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho katika msikiti wa Rahaleo saa nne, kwa mujibu wa taarifa ya watu wa karibu na marehemu.

Mwenyezi mungu amlaze pema peponi

4 comments:

  1. Inna Lillahi Wainna ilayhi Rajiuun.

    Ya Rabbi Mpe safari ya nyepesi, umpe Kauli thabit, umuondoshee mchanga mzito katika kaburi lake shekhe wetu, umkutanishe na waja wako wema aendako. Ya Rabbi wape Subira wafiwa.
    Ya Rabbi tupe na sisi tuliobakia safari njema na Kauli Thabit. Amin

    ReplyDelete
  2. Inna lillahi waina ilayhi Rajiunna, mauti ni faradhi lakini kifo hiki kinaniuma sana, kama nilipofiwa na baba yangu, kwa kweli sheikh huyu sijaona mfanowe hapa visiwani na hofu yangu kwamba tayari zanzibar tumeshampoteza mwanazuoni mkubwa katika zama hizi na pengo lake litakuwa shida kuzibika.

    ReplyDelete
  3. amiin yarabbi inna lillahi wainna ilayhi rajiuun

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.