Habari za Punde

Haroun azihimiza mawizara kufanya tathmini ya kazi zao



Na Kauthar Abdalla
WAZIRI wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman ametoa wito kwa mawizara na taasisi mbali mbali kuandaa mikakati ya ufuatiliaji na kufanya  tathmini ya kazi zao katika shughuli zao za kila siku.

Hayo yameelezwa wakati wa ufunguzi wa warsha ya ufuatiliaji na tathmini iliyofanyika ukumbi wa Ocean View hoteli Kilimani mjini Zanzibar.

Alisema endapo taasisi zitaweza kujipanga kufanya tathmini kwa wanachokifanya kunaweza kuleta mabadiliko na kuondoa kasoro zinazoonekana katika kufikia malengo.


Nae Mwakilishi wa  Shirika la Kazi  Duniani (ILO),Fatma Mohammed Rashid akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo alisema ni vyema taasisi inapofanya kazi ikajitathmni ili kuweza kuleta ufanisi katika kazi.

Pia alisema wameshukuru wizara hiyo kwa mashirikiano katika kufanikisha masuala ya tathmini na ufatiliaji wa masuala hayo.

Nae Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi (ZATUC), Khamis Mwinyi alisema mpango wa ufatiliaji na tathmini unaibua  changamoto mbali mbali hivyo ni vyema kwa wanaohitaji kufanyiwa tathmini hiyo kukubali kwa hiari.

Mapema Mkurugenzi Mipango,Sera na Utafiti, Radhia Rashid alisema lengo la warsha hiyo ni kuandaa mfumo wa tathmin katika kufuatilia utekelezaji wa shughuli kulingana na  mpango mkakati wa wizara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.