Habari za Punde

Papa: Kwaherini

VATICAN, Italia
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict wa XVI amekiri kwamba alikabiliwa na ‘wakati mgumu’ katika kipindi cha miaka minane ya kuliongoza kanisa hilo, lakini aliongoza kutokana msaada wa Mungu.

Papa Benedict (85) aliwambia waumini wa kanisa hilo kutoka kila pembe ya dunia waliokusanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro kumuaga kiongozi wao, katika misa yake ya mwisho kama Papa.

Papa atastaafu rasmi upapa leo na kuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kujiuzulu tokea mwaka 1415 wakati Papa Gregory XII alipojiuzulu.

Mrithi wake atapatikana katika mkutano wa Makadinali (conclave) unaofanyika katikati ya mwezi Machi.

Alisema alikuwa amebeba mzigo mzito, lakini aliukubali kwa sababu alikuwa na hakika kwamba Mwenyezi Mungu atamuongoza.

Aliwashuru waumini wa kanisa hilo kwa kuheshimu uamuzi wake wa kujiuzulu na kusema ataendelea kuwa muumini wa kanisa.

Zaidi ya waumini 150,000 walihudhuria misa yake ya mwisho, wakiwemo wakaazi wa jimbo la kusini mwa Ujerumani la Bavaria anakotokea kiongozi huyo.

Akiwa ndani ya gari maalum la Vatican, Papa aliuamkia umati wa waumini waliojazana katika uwanja wa Mtakatifu Petro,muda mrefu zaidi kuliko kawaida yake kabla ya kuwakaribisha kwa mazungumzo baadhi ya viongozi ikiwa ni pamoja na rais Ivan Gasparovic wa Jamhuri ya Slovakia.

Tangu siku kadhaa zilizopita,umati wa waumini kutoka Ujerumani wamekuwa wakimiminika mjini Rome.

Wenyewe wanasema hata akiacha wadhifa huo leo 28, ataendelea kuwa muhimu kwao.

Tobias Eichinger aliyesafiri hadi Rome pamoja na mchumba wake Cornelia anasema:"Tumekuja kumuombea Papa mtakatifu ambae ni wa kutoka Bavaria na pia ni mwenzetu, kila la kheri.

Madaraka ya Papa yamaliza leo saa 2:00 asubuhi kwa saa za Italia na baadae atasafiri kwa ndege kuelekea kusini mwa Italia karibu kilomita 15 kutoka Vatican kwa ajili ya mapumziko na matibabu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.