Kikosi cha timu ya Bodi ya MapatoZanzibar ZRB, kinachoshiri Kombe la Mabenki, michuano hiyo imeandaliwa na Benki ya Watu wa Wazanzibar PBZ,ili kuimarisha michezo na kujenga ushirikiano wa mabenki Zanzibar kuwa pamoja katika michezo.Michuano hiyo iliofanyika katika uwanja wa Kikujuni Mnazi mmoja ,timu hiyo imefungwa na timu ya Shirika la Umeme kwa mabao 2-1.
Kikosi cha timu ya Shirika la Umeme Zanzibar kilichoizamisha timu ya ZRB, katika michuano ya mabenki uliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja ytimu hiyo imeshinda 2-1
Golikipa wa timu ya ZRB akidaka mpira na hukiu mshambuliaji wa timu ZECO akijaribu kuona ninin kitatokea.
Kikosi cha timu ya Mfuko wa Jamii Zanzibar ZSSF, ambacho kinashiriki kombe la mabenki, kikiaza mashindano hayo kwa kufungwa na timu ya Chuu Kikuu cha Taifa SUZA, kwa bao 1-0. mchezo uliofanyika katika uwanja wa miembeni mnazi mmoja.
Profesa Idris akikimbilia mpira katika mchezo wao wa kwanza na tinu ya ZSSF,uliofanyika katika uwanja wa Miembeni mnazi mmoja, timu hiyo imeshinda kwa bao1-0
Hapa hapiti mtu ndivyo inavyoonekana akisema beki wa timu ya ZSSF.
Mshambuliaji wa timu ya SUZA akimpita beki wa timu ya ZSSF katika mchezo wa Kombe la Mabenki.
No comments:
Post a Comment