Habari za Punde

Uchaguzi wa ZFA hatimae Wafanyika kwa Mbinde katika Uwanja wa Amani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Mdogo wa ZFA Gulam Abdalla Rashid, akitowa maelezo ya uchaguzi huo, kwa wajumbe uliofanyika katika jukwaa la VIP amaan.na kuwashirikisha wajumbe 53 waliohudhuria







Mgombea wa Urais wa ZFA Ravia Idarous Faina akijieleza mbele ya Wajumbe wa MkutanoMkuu wa ZFA wakati akiomba ridhaa zao kumchagua kuchukua nafasi iliowachwa wazi na Makungu baada ya kujiuzulu nafasi hiyo.Ravia ameibuka mshindi kwa kura nyigi za wajumbe 37 wa mkutano huo.
Mgombea wa Urais wa ZFA Rajab Ali Rajab, akitowa sera zake kwa wajumbe wa mkutano mkuu, wakati akiomba kura na kueleza  adhma yake kuporsha kiwango cha Mpira Zanzibar kuazia ngazi ya Juvinal hadi Taifa, na kushirikiana na Wajumbe katika kuendeleza michezoZanzibar.
 Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar Abdalla Juma Abdalla,akijieleza mbele ya Wajumbe waMkutano Mkuu wa ZFA akiomba ridhaa za kuchagulia kuiongoza ZFA katika kipindi hichi, na kuelezasera zake endapo atachaguliwa kuongoza ZFA. katika uchaguzi huo amepata kura 16



  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA Kabila alipata nafasi ya kuuliza maswali katika uchaguzi mdogo wa Chama hicho kwa mgombea kuhusu msimamo wake katika kurekebisha katiba ya ZFA.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA Nassra Juma, akiuliza swali kwa mgombea kuhusu kuimarisha timu ya Wanawake ya Mpira wa miguu Zanzibar.
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wakibadilishana mawazo baada ya kupiga kura ya kumchagua Rais wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA, uliofanyika katika jukwaa la VIP uwanja wa Amaan.

 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wakibadilishana mawazo baada ya kupiga kura ya kumchagua Rais wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA, uliofanyika katika jukwaa la VIP uwanja wa Amaan.

 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wakibadilishana mawazo baada ya kupiga kura ya kumchagua Rais wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA, uliofanyika katika jukwaa la VIP uwanja wa Amaan. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya uchaguzi mdogo. Rais wa TOC Gulam Abdalla, akitowa matangazo ya mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Amaan jukwaa la VIP.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Mdogo wa Rais wa ZFA, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya uchaguzi mdogo. Rais wa TOC Gulam Abdalla, akitowa matangazo ya mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Amaan jukwaa la VIP.
 Mgombea Urais wa ZFA Abdalla Juma, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo, akitowa shukrani kwa wajumbe waliompigia kura na wasio mpigia kura, katika uchaguzi huo na kuahidi kushirikiana na mshindi wa uchaguzi huo Ravia Idarus, kwa kuibuka mshindi kwa kura 37, dhidi yake aliyepata kura 16.    

 Mgombea wa Urais wa ZFA Rajab Ali Rajab, akizungumza na waandishi wa habari baada ya uchaguzi na kutoka kwa matokea ya mshindi wa nafasi ya urais. Na kumpongeza mshindi wa nafasi hiyo na kuahidi kumuunga mkono katika jitihada za kukiimarisha Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar katika kuinua kiwango cha mpira Zanzibar.kama yeye ni mdao wa mchezo huo. Katika uchaguzi huo hakubahatika kupa kura hata moja.
Kocha Msoma akisoma dua baada ya kumalizika kwa zoezi la Uchaguzi Mdogo wa Rais wa ZFA Taifa uliofanyika katika jukwaa la VIP Amaan.
Rais wa ZFA Ravia Idarus wa kushoto akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA waliomchagua kuwa Rais wa ZFA katika uchaguzi mdogo uliofanyika katika jukwaa la VIP Amaan.na kuwashinda wapizani wake Rajab Ali Rajab na Abdalla Juma aliyepata kura 16 na Ravia amepata kura 37.
Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Kikwajuni na Kocha wa Timu ya Small Simba Abdulhani Msoma, akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA Nassara Abdalla na Salum Msabaha, baada ya kumalizika kwa zoezi ya Uchanguzi Mdogo wa ZFA uliofanyika kwa mizengo baada ya wajumbe kukataa kufanyika katika ukumbi wa hateli ya Zanzibar Ocean View Kilimani, inayomilikiwa na aliyekuwa Rais wa ZFA aliyejiuzuri Amani Ibrahim Makungu.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.