Habari za Punde

Majambazi yapora maelfu ya dola Imara Consultant

Na Khamis Amani
WATU wasiojulikana wamevamia ofisi za kampuni ya ushauri ya a Imara Consultant kuiba kasha la kuhidhia fedha ndani yake mkiwa na mamilioni ya shilingi na fedha za kigeni.

Watu hao wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za jadi, walivamia ofisi hizo zilizopo Vuga mjini Unguja baada ya kumuweka chini ya ulinzi mlinzi aliyekuwa amelala juu ya meza.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi Mkadam Khamis Mkadam alisema, tukio hilo lilitokea kati ya saa 2:00 usiku na saa 11:00 ya alfajiri ya Disemba 13 mwaka huu.

Akizungumzia tukio hilo, alisema kabla ya wizi huo, watu hao walivunja geti la nje na mlango wa ndani wa kuingilia ndani ya ofisi hiyo na kuchukua kasha la fedha na kuondoka nalo.

Fedha zilizokuwemo ni shilingi 1,200,000, dola 22,000 za  Marekani 22,000 Euro 3,000 pamoja na riale za Oman ambazo idadi yake hazijajulikana.

Alisema kasha hilo lilionekana limetupwa maeneo ya skuli ya Dimani na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi na kuwasaka wahusika.


Aidha alisema Polisi wameokota maiti ya mtoto mdogo wa kike wa miaka mitano, ikiwa kwenye migomba.

Alisema, maiti hiyo ni ya Iklima Ali Mohammed mkaazi wa Magogoni aliyefariki dunia baada ya kukokotwa na maji ya mvua.

Tukio hilo lilitokea Disemba 16 mwaka huu saa 7:30 mchana na uchunguzi wa daktari ulionesha alifariki baada kukosa pumzi.

Aidha amewataka wananchi kusherehekea sikukuu ya krismasi kwa amani na utulivu, akisema polisi wamejiimarisha kudhibiti vitisho vyovyote vya uhalifu.

Alisema polisi wameimarisha doria za magari, miguu, pikipiki na mbwa kuhakikisha watu wanasherehekea sikukuu kwa utulivu.2 comments:

 1. Hiyo Ndio Faida yakuachiwa Watu Kuingia Visiwani bila ya Passport na kuacha Maeneo ya Bandari Bubu Bila ya Ulinzi maalumu . Unguja na Pemba haikua na wizi wa Majambazi ambao wanapiga risasi au ku-iba Mamilioni ya Fedha.. Siokama na sema kwamba Unguja na Pemba hakukua na Wizi hashaa... Bali kulikua na wizi mdogo mdogo wakuiba kuku, shop-lifting na kuiba kwenye mashamba...

  Wizi unaonekana Unakua Organised na group kubwa za watu wenye Silaha, ni Style za Kibara.. Ndio tulikokua tunasikia Majambazi wameua na kuiba Mamilioni.... Sasa leo hayo yote yamekua yanatokea Unguja katika sehemu mbali mbali.. Hii nikutoka na Muungano ambao umeifanya Zanzibar Mkoa wa Tanganyika. ......Na Watu kutoka Tanganyika ambao wengine hua ni Wauwaji au Majambazi wanaingia Zanzibar nakufanya Ngome...

  2. Jengine mimi sina Imani na Jeshi la Polisi wala JWT, hili JWT wengi wao ni Wakurya ambao hualika jamaa zao wakaingia Visiwani na kuhujumu watu na maisha yao.....

  3. Kanzishwa kwa Bandari Bunbu katika Visiwa vya Unguja kumezidisha wimbi la Majambazi na Criminality- Serikali SMZ CCM -kama wanavosema kwamba wao ndio wanaoongoza Nchi ya Zanzibar basi hawana budi kulichukulia tatizo hili kwa Jicho la kukomesha...

  4. Bandari zote Bubu zinatakiwa zijengwe Ulinzi wa Kudumu pamoja na Nyumba za Wafanyakazi ambao watakua wanapishana kwa zamu na kulinda Mipaka ya Bahari hizo... Hivi ndivo wanavofanya Wenzetu wanaoishi katika Visiwea....

  ReplyDelete
 2. hizo bandari bubu wamewekewa watanganyika kuja kuongeza kura wakati wa uchaguzi kama hujui mbali ya kuwa ni kichocheo cha ujambazi , vyombo vyote na idara zote za muungano ni za makundi ya aina fulani fulani , nia ya kuondoa pasipoti ni kuhakikisha watanganyika wengi waweze kuingia bila pingamizi , sio vibaya wao kuja kama vile sisi tunavyokwenda tanganyika lakini visiwa vyetu ni vidogo kwa eneo ukiachia uhamiaji ovyo tutakuwa hatuna pa kwenda labda huko tanganyika wao wana ardhi kubwa tupu. Nakubaliana mia kwa mia ujambazi ulikuwa haupo znz , na katika miaka ya nyuma huko hata ukisahau kitu chako cha thamani nje ya nyumba amini usiamini unakikuta kiko pale pale ukirudi na kama ulikiacha usiku asubuhi utakikuta kama ulivyokiacha , kama ukipoteza kipochi cha fedha akiokota mtu hupeleka polisi na utapewa , siku hizi hao polisi wenyewe wezi kiama ukipeleka ,si kutwa ukapewa kisago kuambiwa umeiba halafu ukasota rumande shenzi type ili uwaachie wao wagawane.

  ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.