NAIBU waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar,Mhe Zahra Ali Hamad, akiondosha kitambaa kuashiria kuzindua Tangi la
kuvunia maji ya mvua, huko skuli ya Maandalizi Machomanne Chake Chake, ikiwa ni
moja ya shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
TANGI la kuvunia Maji ya Mvua, huko Maandalizi
Machomanne Chake Chake, lililozinduliwa na Naibu waziri wa wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar,Mhe Zahra Ali Hamad, katika katika shamra shamra za
Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
AFISA mdhamini Wizara ya Ardhi Makaazi, Maji na
Nishati Pemba, Hemed Salim Hemed, akitoa taarifa ya kitaalamu juu ya ujenzi wa
tangi la kuvunia maji ya mvua, huko machomanne mara baada ya kuzinduliwa rasmi,
na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, ikiwa ni shamra shamra
za Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WANAFUNZI wa skuli ya Maaandalizi Machomanne
wakimsikiliza kwa makini, Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar,Mhe
Zahra Ali Hamad, wakati alipokuwa akizungumza mara baada ya kuzindua tangi la
kuvunia maji ya Mavua, ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu
ya Zanzibar.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.
ndugu abdi haya mapinduzi unayapa utakatifu jee uliyashuhudia? jee hukusoma chuoni kuwa utukufu ni wa mola pekee , hakuna kingine kinachoweza kuitwa mtukufu au takatifu zaidi yake yeye? huenda ukaona ni kitu kidogo , lakini ukumbuke kuita kitu chochote zaidi ya Mungu kuwa ni kitukufu utakuwa tayari ushamshirikisha Mungu , na kwa hilo halina msamaha kwa mola, nawasilisha kwako na wengineo wote ambao hutumia neno hili 'tukufu' au 'takatifu' . Huenda kwa kutumia neno hilo katika uandishi wako unajaribu kutafuta sifa kwa watawala madhalimu , kumbuka utapoingia kaburini hakuna dr sheni wala yoyote atayeweza kukusaidia , hata kama utazikwa kwa saluti na mizinga na bendera ya nchi kuwekwa juu ya kaburi lako
ReplyDelete