Habari za Punde

Balozi Seif Akutana na Ujumbe wa ALTEC

Makamu wa Pili mwa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta ya Viwanda, Bandari na Viwanja vya Ndege  ya ALTEC hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta ya Viwanda, Bandari na Viwanja vya Ndege ya ALTEC Bwana Ramzan Musipov Ofisini  kwake vuga Mjini Zanzibar. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta ya Viwanda, Bandari na Viwanja vya Ndege  ya ALTEC uliofika ofisini kwake kwa mazungumzo.
Mkurugenzi  Mkuu wa Kampuni  ya Kimataifa inayojishughulisha na uwekezaji katika sekta ya Viwanda, Bandari na Viwanja vya Ndege  ya ALTEC  Bwana Ramzan Musipov  akiagana  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif. (Picha na Hassan Issa wa – OMPR)

3 comments:

  1. Haya tena smz, kutudanga ndio kaziyenu mahodari kutafuta matapeli wakimataifa mkasema wawekezaji, kwani ilekampuni ya kkutoka Africa kusini, imeishia wapi? miaka mitano inaisha mtawaeleza nini ? waznzibari na serakali yenu ya umoja wakitaifa, watanganyika wakipata tanganyika yao, hatokuja kupigakura maratatu, huku znz, maana nawo watakuwa hawajijui watangukia wapi?

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli tumechoshwa na ahadi hewa zinazotolewa aidha na wawekezaji au vyombo vyetu vya khabari.

    Imekua ni kawaida mfanyabiashara yeyote wa nje akija tu, ama kutembea au kuangalia mazingira ya kibiashara vyombo vyetu hukurupuka na kusema " kampuni fukani kuwekeza Z'bar au kujenga hiki au kile"

    Hali kama hizi zinatutia matumaini ambayo hayapo, kwa mfano tuliwahi kusikia makampuni yatakato wekeza ktk kufua umeme wa takataka, uvuvi wa bahari kuu nk. mpaka leo kimya!

    Nadhani iko haja ya angalau kubadili 'staili' yetu ya uandishi kwa kutumia maneno kama vile" kampuni Fulani yaonesha nia ya kuwekeza Za'bar au huenda ikawekeza Z'bar.

    ReplyDelete
  3. msishangae ndugu zangu kwa kawaida waandishi wa habari ni madalali wa wanasiasa , sehemu kubwa ya uandishi ni unafiki na uongo , ni waandishi wachache wa kweli nao hupigwa vita na serikali yenyewe. Waandishi wa habari ni kikundi cha serikali kama vile polisi , jeshi nk , lazima waandike kile kitachowapendezesha mabwana zao. Tunaambi muungano ukivunjike eti utakuja utawala wa ubwana na utwana , kwani sasa haupo? watwana ni kama hawa waandishi , mapolisi , jeshi ambao hulinda watawala ( mabwana)

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.