Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho, akitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kuahirisha kikao cha asubuhi cha maswala na jibu na hutuba ya Uwasilishaji wa Mswada wa Sheria ya Kuweka Masharti ya Usajili na Usimamizi wa Wathamini, uliowasilishwa na Waziri wa Ardhi Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar Mhe Ramadhani Abdalla Shaban.na kuchangiwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kuupitisha kuwa Sheria leo.
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Mhe Hamza Hassan akifurahia jambo wakati akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardh,Makaazi,Maji na Nishati Ndg Alhalil Mirza, wakiwa nje wa ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kikao cha asuhi leo.
Wawakilishi wakitoka ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kikao cha asubuhi baada ya kuchangia Mswada wa Wizara ya Ardhi leo asubuhi.
Waziri wa Kilimo na Misitu Zanzibar Mhe Sira Ubwa Mwamboya akisisitija jambo na Mwakilishi wa kuteiliwa Mhe Marina Thomas, wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa baraza baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.
Mwanasheria Mkuu wa Serekali Zanzibar Mhe Said Hassan Said akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Ndg Alhalil Mirza wakiwa nje ya ujumbe wa Mkutano akitaka ufafanuzi wa kisheria wakati wa michango ya mswada uliowasilishwa na wizara yake katika mkutano wa baraza la wawakilishi leo.
Waziri wa Ardhi,Makaazi, Maji na Nishati Mhe Ramadhani Abdalla Shaban, akimsikiliza
Katibu Mkuu wa Wizara yake Ndg Alhalil Mirza, wakati wa kuahirishwa kwa kikao
cha Baraza baada ya michango ya kuchangia Wizara hiyo iliowasilisha Mswada wa
Sheria ya Kuweka Masharti ya Usajili na Usimamizi wa Wathamini, uliowakilishwa
katika kikao hicho na kuchangiwa na Wajumbe wa Baraza leo asubuhi
No comments:
Post a Comment