Menu

Saturday, July 11, 2015

Mjue mama Amina Salum Ali, Mgombea pekee kutoka Zanzibar kwenye tano bora



CURRICULUM VITAE (Wasifu )
MAELEZO BINAFSI:
Jina: Amina Salum Ali
Tarehe ya Kuzaliwa: 24 October 1956
Uraia: Tanzania
Jinsia: M/Mke 
Ndoa: Nimeolewa  na nimezaa watoto watano
Anuani : S.L.P 4726
Zanzibar, Tanzania
Barua pepe: ahadizetuziendanenavitendo2015@gmail.com

ELIMU:
1979: University of Delhi (India) – B.A Economics
1981:  University of Pune (India) (Symbiosis College of Management) -MBA in Marketing                                 ( Masoko )
1981: Institute of Management Pune, India – Diploma in Financial Management , Operation            Research.
1983: University of Helsinki, Finland – Diploma in Trade and Export Marketing

UZOEFU WA KAZI
1981 – 1982: Mchumi mwandamizi (Senior Economist) Msaidizi Kamishna wa uchumi wa jumla (Macro Economy ) Tume ya Mipango Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar . Majukumu makubwa ni kumsaidia Kamishna katika kupanga mipango ya kitaifa hasa katika     Mipango ya pamoja ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (5 years Joint Plan for Tanzania) Mipango ya jumla ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
1982 – 1983: Mkurugenzi Biashara za Nje – Wizara ya Biashara ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. kushugulikia masuala ya biashara ya nje Zanzibar ,kutengeneza sera za mauzo nje Zanzibar kufanya tafiti ya bidhaa za ziada za kuuza nje na kutafuta matumizi mapya ya bidhaa za Zanzibar zikiwemo viungo kama karafuu ,nazi na mazao yake kama mbata ,mashudu na mafuta ya nazi. Kuratibu mashirikiano na vyombo vya kimataifa vinavyo shgulikia mambo ya mauzo ya nje kama vyombo vya Umoja wa mataifa kama UNCTAD ,ITC na vyombo vya nchi mbali mbali na halmashauri ya Biashara za Nje (TANTRADE) kwa upande wa SMT.
1983-1984: Katibu Bodi ya Biashara Zanzibar (Wizara ya Biashara Zanzibar.) Kushugulikia Tenda za manunuzi ya Serikali kufuatilia mauzo ya bidhaa zote za Serikali zinazouzwa nchi za nje. Kufuatilia tafiti za Masoko kwa bidhaa za Zanzibar na kujua hali ya Masoko nchi za nje na kuandaa takwimu za biashara za Zanzibar na nchi za nje zinazotumiwa na Tume ya mipango ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
1984 – 1985: Mchumi Mwandamizi – Tume ya Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. (i) Kushughulikia fedha za nje na mahusiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na nchi marafiki na mashirika ya kimataifa. (ii) Msaidizi wa Mshauri wa Uchumi wa Zanzibar kushughulikia sheria ya Uwekezaji ambayo ilikuwa ya mwanzo nchini Mashariki ya Afrika (kabla ya nchi zengine kufuatilia katika miaka ya tisini).
1985-1990: Mbunge Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
1985 – 1986: Naibu Waziri wa Fedha – Wizara ya Fedha , Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT).Msaidizi mkuu wa Waziri wa Fedha .kushughulikia masuala ya Uchumi na Mipango , matumizi na mapato ya Taifa pamoja na vyombo vya fedha .
1986 – 1989: Waziri wa Nchi , Wizara ya Mambo ya Nje, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT) anaesimamia Uhusiano wa Kimataifa na wa Kikanda, na vyombo vya Kimataifa na vya kiuchumi kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Afrika (OAU) na Tume ya pamoja Mashirikiano na nchi marafiki. Mwenyekiti katika kipindi chote wa Kamisheni hizo (Joint Commissions) na nchi zote marafiki za Afrika, Bara la Asia kama China, Iran, Urusi, Korea ya Kaskazini, Nchi za Marekani ya kusini kama Guyana, Venezuala, Ulaya ya Mashariki (Bulgaria). Mwenyekiti wa Vikao vya Mawaziri vya Kanda ya PTA sasa COMESA mwaka 1987, na Vikao vya Mawaziri wa SADC mwaka 1988. Mwenyekiti wa Kikao cha Mawaziri wa Fedha na Uchumi cha UNECA mwaka 1987 Ethiopia na Niger. Mwakilishi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye vikao vya G77, Mahusiano ya kiuchumi na nchi za Kusini (South South Cooperation) UNECOSOC, na Mwakilishi kwenye vikao vya nchi za Visiwa.
1989 – 1990: Waziri wa Nchi, Wizara ya Fedha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) Kushughulikia Mahusiano ya Kimataifa na Kikanda na pia kuratibu suala la kulipa madeni tunayodaiwa na nchi marafiki walio nje ya utaratibu wa Paris (IMF, WORLD BANK)
1990 – 2000: Mbunge bunge la Jamhuri ya Muungano
1990 – 2000: Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuteuliwa na Rais na pia Jimbo la Kwahani Zanzibar.
1990 – 2000: Waziri wa Fedha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwa na jukumu la kusimamia Uchumi wa Nchi Msimamizi Mkuu wa Sera ya Mapato na matumizi ya SMZ, Sera za Uchumi na Fedha na ukuaji wa Uchumi na vyombo vya Fedha zikiwemo Mabenki na Mashirika ya nayo husiana.
2001 – 2005: Mjumbe wa Tume ya Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar . Majukumu ya kusimamia sera za Uchumi ya Zanzibar na masuala yote ya Serikali yanayohusu Mipango ya nchi
2005-2006: Mjumbe Baraza la Wawakilishi – nilijiuzulu baada ya kujiunga na AU.
2005 – 2006: Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kushughulikia uratibu wa Serikali, Tume ya Uchaguzi, Baraza la Wawakilishi, Sera ya Uwezeshaji wa wananchi na Mashirika yanayotoa mikopo midogo midogo TASAF, Mkurabita nk. Uratibu wa mashirikiano na Serikali ya Muungano (SMT), Masuala ya Maafa, Masuala ya walemavu, Masuala ya HIV-Aids na Tume ya Ukimwi ya Zanzibar na Uratibu wa mambo ya ndani ya Nchi Polisi na Uhamiaji.
2006 – Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) Marekani (United States) akiwa kama ni Muwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika. (i) Mshauri wa Kamisheni Umoja wa Afrika kuhusiana mambo ya Afrika huko Marekani. (ii) Kufuatilia mambo ya Maendeleo ya Afrika huko Marekani kwa kuwajuilisha kuhusu sera mbali mbali za bara la Afrika zinazoendelea na mpya. (iii). Kuwashajiisha wawekezaji wa Marekani na pia Diaspora wa jamii ya Kiafrika huko Marekani kuwekeza Afrika. (iv) Kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na vyombo vya Serikali, Mabunge na Taasisi za kijamii za Afrika . (v) Kusaidia kupatikana kwa Fedha za Maendeleo ya Afrika kwa kuzieleza Sera za Maendeleo za Afrika, na kuwashawishi waziunge mkono. (vi) Kushirikiana na vyombo vya fedha vya Bretton Woods (World Bank na IMF) kwa Maendeleo ya Afrika. (viii) Kuleta mashirikiano na vyombo vya Elimu ya juu, Mashirika ya Kimataifa, Mifuko ya Maendeleo, Vyombo vya kujitolea na vya hiari (Universities, Research Institutes, Philanthropic Institute Foundations ie Gates, Clinton etc) Kuifahamisha Marekani mambo ya Maendeleo na taarifa njema za kutia moyo na zenye kuleta Maendeleo kwa jamii ya Afrika kwa wamarekani, kwa kutumia vyombo vya habari vyenye Taarifa sahihi.(xv) kuratibu shughuli za ofisi za kibalozi za Afrika kwa lengo kubwa la kuweza kuwa na sauti ya pamoja katika masuala muhimu ya Afrika na maendelo yake pia na mahusiano na serikali ya Marekani

UZOEFU KATIKA CHAMA.
1968: Nilijiunga na Umoja wa Vijana wa ASP (ASP Youth League) na kuendelea na Uanachama hadi kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.
1977: Nilijiunga na Chama Cha Mapinduzi baada ya kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM
1987 – 2006: Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi hadi nilipolazimika kujiuzulu kufuatia kuteuliwa kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) huko Marekani. Mlezi wa Jumuiya ya Vijana Mjini
1992 – 2006: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi hadi nilipojiuzulu kufuatia kujiunga na Umoja wa Afrika (AU)
2003 – 2006: Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wanawake ya Chama cha Mapinduzi , nafasi niliyolazimika kujiuzulu baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Umoja wa Afrika Marekani.
1987 – 2006: Mjumbe wa Kamati mbalimbali zilizoundwa na Chama kwa kipindi chote nilichokuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi.
Mlezi wa mkoa Morogoro.
Mlezi wa umoja wa vijana Zanzibar wilaya ya Mjini.

SHUGHULI ZA KIJAMII.
1990: Mwanzilishi wa Jumuiya isiyo ya Kiserikali (NGO) ya kwanza kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake (Catalyst Organisation for Women Progeress in Zanzibar)
1995: Mwanzilishi wa Zanzibar Welfare Trust, na pia nimekuwa mlezi wa Zanzibar NGO Clusters.
Aidha nilkuwa Mwanzilishi wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Mwanzilishi wa mfuko wa Rais wa Kujitegemea

BODI MBALIMBALI.
1992 – leo Mwenyekiti wa Jumuiya isiyo ya Kiserikali ya kuendeleza Wanawake Zanzibar (Catalist Organisation for Women Progress in Zanzibar) –COWPZ
1992-1995 Mjumbe Bodi ya Biashara za nje Wizara ya Biashara na Viwanda SMT.
1996 – 1999: Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Magazeti ya Chama Uhuru na Mzalendo
2002- 2005: Mjumbewa baraza la chuo kikuu Cha mzumbe (Mzumbe university council)
2003 – 2004: Mjumbe wa Bodi ya Biashara ya Nje, Wizara ya Biashara na Viwanda – Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
2003 – 2005: Mjumbe wa Mfuko wa Elimu Zanzibar, Wizara ya Elimu Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar.
2004 – 2005: Mjumbe wa Bodi maalum iliyoshughulika na kazi za Maendeleo ya Wanawake katika Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (JEDDAH)
2004 – 2006: Mdhamini wa Jumuiya zisizo za Kiserikali Zanzibar (Zanzibar NGO Clusters – ZANGOC zinazoshughulika na masuala ya Ukimwi (HIV – AIDS)

LUGHA:
 Kiswahili na Kiingereza – Kuongea na Kusoma kwa Ufasaha





 
 Tunaomba na Tanzania tuwe na 
Madam  President
 Nakuahidini Taifa  Stars Nitafanya kila niwezalo kama mungu 
atanijaalia kuwa  Rais muwe  katika timu 10 bora za mataifa ya Africa
















 Jemedari wa  Chama  

Balozi  Amina Akiwa na  viongozi REFTO baaada ya kuwasili  kwenye mualiko leo hii.
 
Balozi  Amina  akizungumza  na wanajumuiya leo hii. 




Balozi Amina akikabishi fomu baada ya
 kukamilisha wadhamini wote.
 



 Balozi  Amina  akiwa  Geita.





Balozi Amina  akiwa Bukoba kkamilish  kazi.













Balozi Amina akiwa Zanzibar kukamilisha 
wadhamini Moshi.




Balozi Amina akiwa Zanzibar kukamilisha 
wadhamini Mkoa wa  Pwani.












 Balozi Amina akiwa Zanzibar kukamilisha 
wadhamini kwa  upande wa Mtwara na  Lindi.

 Balozi Amina S.Ali awasili Uwanja wa  ndege wa Pemba
Balozi  Amina  akikamilisha  kazi ya kuwapata wadhamini Pemba.


Balozi Amina  alipokuatana na mgombea  mwengine wa CCM kutaka ridhaa ya kupitishwa kugombea urais wa Tanzania Mhe Samuel Sita katika Uwaja wa  ndege  wa Pemba.

Ahsanteni wazee na vijana wote huko Pemba tunaokwenda pamoja na Mama Amina.

 
Balozi Amina  baada ya kumaliza kazi Pemba.

  

Kinana  Zanzibar wakiwa kwenye  furaha kubwa ya kuwa na Balozi Amina  S.  Ali.



HOTUBA YA BALOZI AMINA SALUM ALI YA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA, JUNI 3,, 2015

Ndugu wana habari
Wananchi wote mnaonisikiliza
Mabibi na Mabwana

Habari za mchana,

Niliyesimama hapa mbele yenu naitwa Amina Salum Ali.
Mimi ni mzaliwa wa Tanzania, kwa upande wa Zanzibar. 
Ni Mtanzania Mzaliwa wa Zanzibar, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Ndugu zangu, nimewasili hapa mjini Dodoma kutoka Zanzibar ili kutimiza dhamira na kwa kweli nia na kusudio langu la siku nyingi la kukiomba chama changu cha CCM kinipatie fursa ya kuiongoza nchi yetu kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Kutokana na azma hiyo, awali ya yote, hususan kabla ya tendo hilo la kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa katika nchi yetu na CCM, ni vizuri kwangu kuwaeleza kile ambacho kimekuwa kikinisukuma kuchukua fomu ya kuomba Chama changu cha CCM kiridhie na hivyo kubariki kusudio langu la kuiongoza nchi yetu katika awamu ya tano ya utawala katika nchi yetu.

Kwanza, mimi ni Mtanzania wa kuzaliwa na ni Mwanachama na mmoja wa wanachama waanzilishi wa_CCM-- ndio maana nachukulia fomu hapa makao makuu ya kitaifa ya CCM! 

Kwa kipindi cha miaka takribani arobaini iliyopita nimebahatika kuwa mjumbe wa kamati mbalimbali ndani ya CCM kiasi ambacho kwa sasa naifahamu fika katiba yake na malengo kitaifa na kimataifa.


Pili, natambua kazi ya kuiongoza nchi si lele mama. Ni kazi kubwa inayohititaji nia ya kweli, uwezo, uzoefu, na uadilifu wa kutosha ukibarikiwa na kusimimiwa na Mwenyenzi Mungu. Kwa kutambua haya napenda kuuthibitia uma wa Watanzania kwa kupitie nyie Wanahabari kwamba: 

Nia ya kuiongoza nchi yetu Ninayo, tena sana. Mtakumbuka mwaka 2000 nilijitokeza kuchukua fomu ya kukiomba Chama cha Mapinduzi (CCM) kinipatie fursa ya kuiongoza nchi yetu. Ombi langu kwa wakati ule halikuwa riziki. Kwa mara hii ya pili sasa, najitokeza tena ili kukiomba Chama cha Mapinduzi kinipatie fursa ya kutimiza nia yangu hiyo ya miaka ishirini iliyopita ya kuiongoza nchi yetu kama Raisi.

Ndugu zangu Wanahabari, Uwezo ninao wa kuihudumia nchi yetu katika nafasi hiyo ya juu kabisa ya kiutawala katika nchi yetu.  Kwanza ninayo elimu ya kutosha kunipa kuyatambua, kuyaelewa na kuzifanyia kazi changamoto zilizopo nchini mwetu kwa sasa.  

Uzoefu ninao: Aidha kwa ridhaa ya CCM na/au Serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serilali ya Mapinduzi ya Zanzibar nimepata uzoefu, tena mkubwa, kwa kushiriki, kuhudumia au kuwakilisha nchi yetu katika nafasi za uongozi za kitaifa na kimataifa. 

Ndugu zangu, mtakumbuka ule usemi maaraufu Rais John F. Kennedy, ambaye alikuwa Raisi wa 35 aliyetawala Marekani tangu mwaka 1961 hadi alipouwawa mwaka 1963, alipata kuwaambia Wamerekani wenzake: “Msiuulize Marekani iwafanyia Nini, Ila mjiulize mtaiifanyia nini Marekani.” Maneno hayo ya hayati Raisi Kennedy (Mungu amlaze vyema peponi) kwangu mimi yamekuwa yakinipa changamoto kubwa na kwa siku nyingi---ni kitu gani ninataka na ninaweza kuifanyia nchi yangu ili kuipatia maendeleo ya haraka ya watu na vitu.. 

Ndugu Wanahabari, kutaka kwangu kuiongoza nchi yetu si kutaka tu. Ila KUNATOKANA na kutambua vyema na kutaka kuchangia kuondokana na changamoto nyingi na kubwa za kiuchumi, kisiasa, na kijamiizilizopo nchini mwetu; na pili changamoto za kufanyia kazi kwa haraka zitokanazo na mashirikiano ya nchi yetu nan nchi nyingine vile vile mashirika ya Kimataifa.  

Kati azma ya kuomba ridhaa ya kuiletea nchi yetu maendeleo,   leo hii Nimeamua kuchukua fomu ya kuiomba CCM inipatie fursa ya kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa nina nia dhabiti, uwezo na uzoefu wa kutosha kabisa kusimamia sera na mikakati ya kupambana na changamoto za maendeleo zilizopo ili kulipatia Taifa letu maendeleo makubwa, ya juu na ya haraka.

Azma hiyo inawezekana  kwanza, kwa kuyaendeleza na kusimamia yale yote mazuri ambayo yametokana na uongozi wa Serikali ya awamu ya nne; na pili, kwa kubuni sera, mikakati, mipango, sheria na taratibu mpya za kuendelea kuutayarisha uchumi wetu kukua na kufikia kuwa nchi ya kiwango cha kati au cha juu cha maendeleo ya watu na vitu. Tatu ni kuzipa kipaumbele sekta na maeneo ambayo yatachangia kutatua changamoto za kiuchumi, kisiasa, na kijamii zilizopo nchini mwetu. Maeneo hayo ni kama yafuatayo:

KUONGEZA KASI YA UKUAJI UCHUMI KWA KUPANGA UPYA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO KWA KUTUMIA VIZURI RASILMALI ZA NCHI ILI ZIWANUFAISHE WANANCHI.

Tanzania ina rasilmali za kutosha kwa ajili ya leo na kwa kizazi kipya. Malengo ya serikali  ni kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati.Ni dhahiri inaonesha kwamba kuna haja ya kuwa na mapinduzi ya kifikra na kimkakati kwa kupitia upya Dira yetu ya maendeleo 2025 kwa kuweka mikakati  madhubuti ya kufanya mapinduzi ya kutufikisha kwenye uchumi wa kwanza katika mpango wa muda mrefu kupitia katika uchumi wa  kati.
Kuna haja ya kuwa na chombo maalum cha kusimamia masuala ya uchumi na maendeleo katika nchi yetu. Chombo hicho maalum ambacho kitasimamiwa na uongozi wa juu kitaifa kitakuwa na jukumu la kutoa ushauri wa haraka kuhusu maeneo na aina ya uwekezaji unaohitajika ambao utachangia haraka kukua kwa uchumi na upatikanaji wa ajira nchini mwetu.  Pia chombo hicho kitasaidia sana  kuondosha ucheleweshwaji wa maamuzi  ya uwekezaji, kuondoa mikataba mibovu na ya hasara na isiyo na tija kwa taifa letu,  na pia kitasaidia kuziba mianya ya rushwa na ufisadi. Naamini mashirikiana kati ya chombo hicho kipya cha uchumi na maendeleo na Tume ya Mipango kutachangia haraka ukuaji wa uchumi utakaomgusa kila Mtanzania.  

kipaumbele kitawekwa kwa sekta zitakazochangia haraka na moja kwa moja kupunguza umasikini, kwa mfano, kilimo na viwanda, Kwa sababu hii Serikali itabuni njia bora za kukuza uhusiano kati ya uwekezaji na ukuaji wa viwanda na kilimo, kuanzia wakulima na wajasiriamali wadogo wadogo hadi wakulima na viwanda vikubwa vya kusindika mazao ya kilimo. Naamini, kwa kufanya hivyo kukua kwa uchumi na maendeleo ya kiuchumi yatawagusa wanachi kwa kuwapatia tija katika uzalishaji mali na hivyo kuwapatia kipato kingi na cha kutosha kujikimu na kuweka akibaya kujipatia mahitaji na huduma za msingi, kama vile afya, elimu, na makazi bora.

njia kuu za usafirishaji, ikijumuisha reli, barabara, na usafiri wa baharini na maziwa, ama zitafufuliwa au kujengwa upya ili ziweze kuchangia haraka kukua kwa uchumi na pia kulinda uchumi wetu dhidi ya mfumuko wa bei.  Sisi sote tunatambua  kwamba nchi yetu bado ina uhitaji mkubwa wa njia nzuri na salama za kusafirisha watu na mizigo. Naamini kwamba uimarishaji wa miundo mbinu ya usafirishaji utaongeza uhitaji wa bandari zetu katika nchi jirani na hivyo kutupatia fursa ya kupatia kipato na kuhimarisha mahusiano ya kidugu ambayo ni ya muda mrefu sasa.


KUPUNGUZA KWA KASI UMASKINI  NA KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA  

Lengo hili nitalisimamia kama ifuatavyo:

Kubuni sera na mikakati ya kupunguza kwa kasi ndani ya muda mfupi umasikini unaowaathiri sehemu kubwa ya wananchi kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya 2025. Kuleta Mapinduzi ya dhati katika sekta muhimu zinazoleta maendeleo ya haraka kwa wananchi. Mapinduzi hayo yatatokana na matumizi ya teknolojia za kisasa uzalishaji katika sekta zote kuu za kiuchumi, hususan kilimo, ufugaji, na uvuvi, ikisaidiwa sana na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano, na kuwawezesha wakulima, wafugaji, na wavuvi waweze kuuza ndani na nje ya nchi na/au kuuzia viwanda vitakavyoanzishwa au vile vilivyopo nchini.

Kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza ukuaji wa uchumi kwa kukaribisha na kushirikiana na sekata binafsi katika kufufua viwanda vinavyotumia mali ghafi itokanayo na kilimo, mathalan, pamba, korosho, maziwa, matunda, na, alizeti. Pia nalenga kusimamia kuchakatwa kwa mali ghafi, madini na vito ili kuviongezea thamani kwa kutumia viwanda vilivyopo au vitakavyojengwa nchini mwetu.  Ili kuchangia haraka upatikana wa ajira kwa vijana, hasa wanawake, viwanda vitakavyoanzishwa nchini mwetu vitasimamiwa au kuongozwa vyema ili view na mahusiano ya kiuchumi na yatakayoto chngamoto za uwezekezaji katika sekta na maeneo mengine ya nchi yetu.    

KASI YA,UWEZESHWAJI KWA WANAWAKE NA Familia  .KUTOA MATUMAINI MAPYA KWA KIZAZI KIPYA

Nchi yetu ina idadi kubwa ya wanawake. Takwimu zinaonesha idadi ya wanawake wote wa Tanzania ni takriban milioni 25, yaani zaidi ya nusu ya Watanzania wote, wanaohitaji kutambuliwa na kupewa fursa sawa kwa kushirikishwa kikamilifu katika upangaji wa matumizi ya rasilimali za kitaifa. Hili linawezekana kwa wanawake kushirikishwa au kuwezeshwa kushiriki katika mipango yote ya maendeleo ya kiuchumi kijammi na kisiasa hasa katika maeneo ya kutoa maamuzi yaayogusa jamii. Kwa hiyo basi, Serikali yangu itapigania kuondoa kasoro za mfumo dume ambao bado unachangia kudumaza huduma za msingi kwa wanawake, kwa mfano Elimu, ili tupate maendelo ya haraka. 

Mimi ninaamini, kwa wingi wao, mkakati wa kumuendeleza na kuwainua kimaendeleo mwanamke wa Kitanzania utakuwa ni njia nzuri pia ya kuwainua Watanzania kutoka katika ufukara wa kipato, kielimu, n.k. Usemi uliotawala kati yetu ambao ni wa kuuzingatia ni kwamba: Ukimwendeleza mwanamke utakuwa umeendeleza jamii.


KUKUZA UTOAJI WA HUDUMA  ZA JAMII KWA USAWANA KWA WOTE

Kwa miaka takriban 50 sasa nchi yetu bado inagubikwa na tatizo la huduma duni kwa jamii, kwa mfano utoaji wa afya na kinga za mama na mwana ili kupunguza vifo vya wazazi na watoto walio chini ya miaka mitano. Ukosefu wa huduma muhimu katika utoaji wa afya na kinga za mama na mwana ili kupunguza vifo vya wazazi na watoto walio chini ya miaka mitano. Serikali imechukua hatua kubwa sana za kupeleka huduma za afya kwa wanachipia imejitahidi kutafuta ufumbuzi wa kushughulikia matatizo ya sekta hii. Hata hivyo bado hatua za ziada zinahitajika hususan kwa kuwekeza katika hospitali zetu kwa kuwa na zana zinazohitajika na pia kuwa nadawa ya kuwahudumia wagonjwa wanapo hitaji.suala la madaktari na wafanya wa sekta ya afya ni la msingi kabisa ni muhimu kutafuta mkakati wa kuwapa motisha na vitendea kazi waweze kutoa huduma muafaka.hivyo kero walizo nazo ni muhimu zipatiwe ufumbuzi wa haraka.sera ya afye kwa wote itizamwe upya na iwe ni sekta ya uwekezaji badala ya mtizamo wa sasa kwamba ni kitengo cha huduma kwa wananchi kwa misingi hiyo utaratibu maalum uwepo wa kuongeza mtaji katika sekta hii ya afya kwa kuwasajiisha wawekezaji wan je na ndani kuwekeza kwa kujenga hospitali za kisasa ,zenye vifaa vya kisasa vya kutolea huduma na watendaji mabingwa  ambao hivi sasa tunao ambao wengi wao wamevunjika moyo .Pia kushajiisha vituo vya utafiti vya masuala ya afya na huduma mbali mbali. Vifo vya mama na mtoto vimepunguwa lakini bado vinahitaji vipunguzwe Zaidi. Kwa hiyo basi kuna sababu za kimsingi kabisa za kusimamia vyema au kubuni sera na mikakati bora zaidi itakayopelekea kuwepo nchiniu upatikanaji wa huduma bora za jamii, kwa usawa, kwa wote na kwa unafuu.

MGAWO BORA WA PATO LA TAIFA

Kwa miaka kumi iliyopita pato la nchi yetu limekuwa likiuwa kwa kiwango kinachoridhisha. Hata hivyo, ukuaji huo wa pato la taifa haujaambatana na kuwaletea maisha bora Watanzania walio wengi.  Taifa letu limekuwa sasa kama linakubikwa na hulka ya aliyenacho kutojali au kumjua asienacho angali tofauti ya kipato na maisha kati ya Watanzania ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwangu mie tofauti hiyo kubwa ya kipato katika jamii ya Kitanzania ni hatari kwa mustakbali wa umoja wa kitaifa na amani na utulivu wa kuletea nchi yetu maendeleo. Kuna sababu ya kimsingi inayohitaji utekelezaji wa haraka wa kuwepo mgawo bora wa pato la taifa ili Mtanzania wa kawaida aweze kujikimu kimaisha. Hili linawezekana kwa Serikali kurekebisha viwango vya kodi zinazolipwa na watu wa kipato cha chini; kwa Serikali kusimamia vyema sekta binafsi ilipe kodi stahiki na kwa viwango vilivyowekwa; kubuni sera na taratibu bora zaidi za kuiendesha na kuiwezesha mifuko ya inayowahudumia wastaafu; na kubuni na kuendesha mifuko ya kuwahudumia wazee, kina mama walioachiwa majukumu makubwa kutokana na kuwapoteza wenzi wao aidha kwa ajali, ukimwi, n.k.;  Utaratibu huu utafanikiwa kwa kuangalia upya ulipaji na ukusanyaji wa kodi na kwa kuwa na njia nyingine za mapato.  Vile vile ni tutaangalia upya ulipaji wa kodi wa walipaji wa kipato cha chini ili kudhihirisha azma yetu ya kuwa Taifa   linalojali watu wake, wakiwemo wanawake, vijana, wazee, walemavu wote, ikijumuisha wale wenye ulemavu wa ngozi. Vipofu, viziwi, mtindio wa ubongo, n.k. Katika uongozi wangunitatoa kipaumbele kwa kupunguza tofauti hizo na kuwaangalia kwa kina maskini na wenye vipato vya chini walio wengi kwa kuwapatia uwezo na njia mbadala za kuweza kukimi maisha.

ELIMU

Kuporomoka kwa ubora wa elimu katika ngazi zote ni changamoto kubwa nchini mwetu. Sehemu kubwa ya wahitimu wetu wamekuwa wasio na uwezo au elimu ya kutosha kupata au kuijipatia ajira wao wenyewe ili waweze kujikimu kimaisha, Vile vile elimu yao haiwawezeshi kukabili kikamilifu ushindani katika soko la ajira ndani nan je ya nchi yetu.  Wakati umefika sasa wa kuinua kiwango cha elimu kwa kuangalia upya mitaala ya kufundishia na kuwaandaa vyema waalimu bora na wa kutoosha kufundisha kuanzia elimu ya chekechea hadi ya vyuo vya elimu ya juu. Kwa serikali kusimamia vyema na haraka uwepo wa kiwango bora cha Elimu tutakuwa tumewaongezea vijana wetu uwezo wa kuajiriwa humu humu nchini au nchi nyinginezo zilizo ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Serikali yangu itapigana kuvutia wawekezaji makini au itashirikiana na sekta binafsi kuwekeza katika elimu.  Vipa umbele vitapewa katika elimu itakayojenga vipaji na na kuwaongezea wahitimu utaalam wa kutosha na unaohitajiwa katika taifa, hususan kwenye sekta mpya za mafuta na gesi asilia; kuwapatia elimu ya stadi maalum; kuongeza wataalam na mabingwa  wa fani mbali mbali kwa wakati tulionao ili uchumi ukue kwenda uchumi wa kwanzakupitia  wa kati. Hii itawezekana kwa kubuni mitaala ya kuwafundishia wataalaa njia bora za kufundishia na kuwafundisha watoto wetu ujasiriamali ili waweze kujiajiri pale wamalizapo masomo.

UTAWALA WA SHERIA

Kuweka mazingira bora ya kisheria ya kuwezesha uwekezaji katika uzalishaji mali na kuendesha biashara na miradi mikubwa nchini mwetu ili kukuza haraka ukuaji uchumi na kushinda vita dhidi ya umaskini. Ingawaje sote tunakubali mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi wan chi yetu, sekat hiyo inahitaji kusimamiwa vyema kwa wawekezaji wa nje kuwekewe mazingira mazuri na utaratibu maalum kwanza wa kuwekeza na pili kuingia ubia na wawekezaji wa ndani katika utekeleza wa miradi mikubwa ya kitaifa. Pia inabidi sasa kuwa na sheria zilizo za wazi ambazo zitawapatia wawekezaji wa ndani utaratibu wa kurahisisha shughuli zao. Ili ili litokee, Serikali yangu itajikita kusimamia vyema, au kuzifanyia mapitio yatakayolenga kuboresha na ikibidi kubuni sheria mpya za uwekezaji na kusimamia uendeshaji wa biashara ambazo zitaendana na mfumo wa uchumi utakaoendana na dira ya maendeleo ya taifa .

ULIPAJI NA UKUSANYAJI KODI

Takwimu za kitaifa zinaonyesha bayana kushuka kwa ukusanyaji wa kodi nchini mwetu mwaka hadi mwaka tangu mwishoni mwa miaka ya tisini (1990s). Mapungufu ambayo yamekuwa yakijitokeza katika ukusanyaji wa kodi yamekuwa yakileta adha nyingi kwa serikali n ahata watanzania, kwa mfano, kushuku au kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii, kuchelewa kwa mitihani, kutopatikana kwa haraka mikopo ya wanafunzi, wakulima kutolipwa mapema mauzo ya mazao yao, n.k. 

Serikali yangu itaimaarisha vyombo, taratibu na sheria zinazosimamia ukusanyaji wa kodi na mapato mengineyo.  Aidha sheria mpya au zilizopo zitasimamiwa kwa ukali na busara ili kufuta kabisa nchini ukwepaji wa kodi. Sambamba na hili kwa Kuweka mazingira bora ya kisheria. Serikali itaweka utaratibu mzuri wa kukusanya kodi na pia kupitia upya maeneo ya vyanzo vya kodi, kuweka uwazi katika ukusanyaji wa kodi ,kuwa na viwango vya kodi vinavyotabirika na vinavyoendana na ukuaji wa uchumi na huduma mbali mbalikuboresha utendaji katika idara za mapatokwa kuwa na ufuatiliaji na ukusanyaji taarifa za wakwepaji wa kodi na kuchukuliwa hatua   kali za kuwabana na kuwaadhibu.. 



RUSHWA, UFISADI, UWAJIBIKAJI NA UKOSEFU WA MAADILI

Rushwa, ufisadi, uwajibikaji usioridhisha, na ukosefu wa  maadili ni mambo ya msingi kwa taifa linalofuata sera ya uwazi na utawala bora  na maadili mema. Tanzania imeingia doa sana kutokana na kugubikwa na vitendo vya ufisadi, rushwa, na mapungufu makubwa ya ukosefu wa uadilifu na uwajibikaji serikalini takriban katika ngazi zote. 

Mimi naamini, Serikali ni lazima iwe inawahudumia wananchi wake wote kwa kusimamia upatikanaji wa huduma bila ya ufisadi na vitendo vya rushwa. Kwa kufanya hivyo, wananchi watakuwa na imani na serikali yao. Kwa bahati mbaya vitendo ambavyo vimekuwa vikiendelea hivi sasa ni vile vya kulindana,  kupendeleana, kutofuata maadili ya uongozi. Kazi kubwa iliyopo mbele ya serikali nitakayounda ni ya kupiga vita rushwa, ufisadi, ukosefu wa uwajibikaji kazini, ukosefu wa maadili serikalini na ndani ya jamii yetu. Vita hivyo ni vigumu na vinahitaji moyo na kuungwa mkono na watanzania wote wenye uchungu na nchi yao. Vita hivyo vitajumuisha kuwepo usimamiaji mzuri na wa karibu wa vyombo vya kusimamia maadili kwa kuvipa pia meno na kupitia upya sheria zake. Mahakama maalum itawekwa ya kushughulikia masuala yote ya rushwa na ufisadi na ubadhirifu wa mali za uma ili sheria kali na stahiki zitolewe kuadabisha wahusika wawe na adabu na kuwa fundisho kwa wengine. Njia hizi ni lazima ziwepo ili tuweze kujenga tabia na utamaduni mpya wa kuchukia rushwa, uzembe, na ufisadi na pia kuweka misingi ya watu kujitegemea na kuishi kwa kutumia njia halali za kujipatia kipatao badala  ya kutajirika haraka kwa ufisadi na hongo.

MUUNGANO NA KATIBA

Nikipewa ridhaa na chama change cha CCM nitaendeleza mchakato wa kupata katiba mpya ambao ulisimamiwa na serikali ya awamo ya nne.Mimi ni muumini wa uhakika wa utawala bora kwa kuamini kuwa katiba inahitaji ridhaa ya wananchi na ndio makubaliano yanayowekwa ili kiongozi wanch na utawala unatakiwa uyatekeleze.Hivyo katiba iliyo bora itatuvusha taifa letu kwenda katika hali ya juu ya maendeleo na amani na utulivu. Katika katiba ni vyema masuala ya liokuwa kero yanaondosha ili kuwa na muungano imara .Muungano ni muhimu sana kwa taifa letu la Tanzani  bado ipo haja ya kuufanya upendwe na wanachi ili wajisikie kuwa ni wahusika na wadau wakuu wa kuulinda usivunjike na kupitishwa kwenye misuko suko isio na manufaa na tija.kuwepo na mikakati maalum ya kufanya mambo yatakayo fanya wananchi wa pande zote mbili wafaidike na waone faida ya kuwa jamii moja .naelewa hii sio kazi rahisi inahitaji nia na dhamira ya makusudi ya kuona mungano unadumu.mimi nimekulia ndani ya muungano , nimefanya kazi ndani ya muungano katika serikali zote mbili nnaelewa change moto ziliopo na zitakazo endelea kuwepo.Mara nyingi ni vikwazo visivyo vya msingi vinazuia kuimarika muungano wetu .binafsi ni muumini kabisa wa hatima ya Tanzania yenye maendeleo ndani ya mungano uliopo. Ndio maisha yetu na maendeleo ya vizazi vyetu. 

LUGHA   
Lugha ya Kiswahili inayotumika nchini mwetu kwa ajili ya mawasiliano ya aina mbali mbali n ahata kufundisha katika shule nchini mwetu ni moja ya tunu na nguzo zinazotuweka kuwa  taifa letu  moja lenye umoja, upendo, na mshikamano ambao umetupatia kuwa na  amani na usalama nchini mwetu kwa muda  mrefu sasa.  Kwa sabau huu pekee Kiswahili kinatakiwa kiendelezwe kudumishwa kama lugha ya Taifa letu. Hata hivyo kutokana na kuongezeka kwa mashirikiano ya kibiashara, kisiasa na kitamaduni kati ya nchi yetu na nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara inabidi pia tusimamie ufundishaji bora wa Kiswahili ili kiwe nyenzo ya kuwapatia vijana wetu ajira, mathlan, kwa kuajiriwa kufundisha, kutoa huduma ya ukalimani, au kwa kuwekeza katika miradi ya shule za kufundisha Kiswahili hapa ndani na nje ya nchi yetu kwa 

MUSTAKABALI WA KITAIFA

Tanzania inapita katika kipindi kigumu. Taifa letu lina mpasuko katika misingi ya dini, ukabila, ukanda, uhasama utokanao na ufuasi wa vyama vya kisiasa, hasa katika vipindi vya uchaguzi. Hali hii inatishia mustakabali mzima wa taifa na maendeleo ya nchi yetu. Wakati umefika sasa wa kukemea kwa nguvu zote na kuweka sheria zitakazoleta na kukuza  masikilizano, malumbano, na mashauriano ya amani ambayo yatajenga  na kudumisha umoja wa kitaifa katika nchi yetu. Naamini kwamba umoja wa kitaifa utawezesha  taifa letu kufanya mambo makubwa ya kujenga uchumi imara na endelevu ambao utapunguza sanaumasikini. 

Tukumbuke pia kwamba kwa muda mrefu nchi yetu ilijikita kusimamia upatikanaji wa uhuru katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Ni wakati muafaka sasa wa kurudisha hadhi ya taifa letu katika usikani wa  uongozi na kusukuma upatikanaji wa maendeleo katika ukanda Afrika na ulimwengu kwa ujumla. 

HITIMISHO

Ndugu wana habari napenda kuhitimisha kwa kusema kwamba kama nikipata ridhaa wa kuwa mgombea wa CCM na baadaye kura zikatosha katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Uraisi wan chi yetu nitapigania kwa nguvu zote maendeleo ya nchi yetu, yaliyoegemea kupunguza umaskini, kukuza upatikanaji bora, kujenga miundo mbinu bora, kujenga na kusimamia utawala wa sharia.  Serikali nitakyoiunda haitamuonea mtu asie na hatia na haitampendelea mtu kwa sababu za urafiki, ukanda, ukabila, udini na jinsia. Vile vile serikali hiyo haitavumilia hata kidogo vitendo vya uvunjaji amani na usalama na vitendo vya rushwa na hujuma wataifa na uvujaji au matumizi mbaya wa rasilimali za nchi yetu kutokana na mikataba mibovu. Hatua madhubuti zitachukuliwa kwa wakati ili kutoa haki stahiki bila ya kuchelewa. Naamini kwamba inabidi sasa tuanze tena kujenga utaifa, uzalendo na utamaduni wa uadilifu, na uwajibikaji katika nchi yetu.  

Kauli Mbiu: Matumaini Mapya kwa Kizazi Kipya 

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Mapinduzi Daima.


Balozi  Amina akikabidhiwa fomu iliosainiwa na wadhamini wa Mkoa wa Morogoro 
katika eneo la Dakawa
Balozi  Amina  akipokelewa na  wana  CCM mbalimbali katika eneo  la  Visiga
Balozi Amina S. Ali akisalimiana na Rais Kikwete .
MwanaDiplomasia Balozi Amina akipeperusha Bendera   ya African Union huko Washington.

Balozi  Amina S. Ali akamilisha wadhamini 45. Hapa ni Ofisi ya CCM  Visiga.

Mama: Amina Salum Ali.

CURRICULUM VITAE  (Wasifu ):
MAELEZO BINAFSI:
Jina: Amina Salum Ali
Tarehe ya Kuzaliwa: 24 October 1956
Uraia: Tanzania
Jinsia: Mke, nimeolewa  na nimezaa watoto watano.

Anuani : S.L.P 4726
Zanzibar, Tanzania
Barua pepe: ahadizetuziendanenavitendo2015@gmail.com
ELIMU:
1979: University of Delhi (India) – B.A Economics
1981:  University of Pune (India) (Symbiosis College of Management) - MBA in Marketing                    
1981: Institute of Management Pune, India – Diploma in Financial Management , Operation            Research.
1983: University of Helsinki, Finland – Diploma in Trade and Export Marketing.
UZOEFU WA KAZI:
1981 – 1982: Mchumi mwandamizi (Senior Economist) Msaidizi Kamishna wa uchumi wa jumla (Macro Economy ) Tume ya Mipango Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar . Majukumu makubwa ni kumsaidia Kamishna katika kupanga mipango ya kitaifa hasa katika Mipango ya pamoja ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
 (5 years Joint Plan for Tanzania) Mipango ya jumla ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
1982 – 1983: Mkurugenzi Biashara za Nje – Wizara ya Biashara ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. kushugulikia masuala ya biashara ya nje Zanzibar ,kutengeneza sera za mauzo nje Zanzibar kufanya tafiti ya bidhaa za ziada za kuuza nje na kutafuta matumizi mapya ya bidhaa za Zanzibar zikiwemo viungo kama karafuu ,nazi na mazao yake kama mbata ,mashudu na mafuta ya nazi. Kuratibu mashirikiano na vyombo vya kimataifa vinavyo shgulikia mambo ya mauzo ya nje kama vyombo vya Umoja wa mataifa kama UNCTAD ,ITC na vyombo vya nchi mbali mbali na halmashauri ya Biashara za Nje (TANTRADE) kwa upande wa SMT.
1983-1984: Katibu Bodi ya Biashara Zanzibar (Wizara ya Biashara Zanzibar.) Kushugulikia Tenda za manunuzi ya Serikali kufuatilia mauzo ya bidhaa zote za Serikali zinazouzwa nchi za nje. Kufuatilia tafiti za Masoko kwa bidhaa za Zanzibar na kujua hali ya Masoko nchi za nje na kuandaa takwimu za biashara za Zanzibar na nchi za nje zinazotumiwa na Tume ya mipango ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
1984 – 1985: Mchumi Mwandamizi – Tume ya Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. (i) Kushughulikia fedha za nje na mahusiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na nchi marafiki na mashirika ya kimataifa. (ii) Msaidizi wa Mshauri wa Uchumi wa Zanzibar kushughulikia sheria ya Uwekezaji ambayo ilikuwa ya mwanzo nchini Mashariki ya Afrika (kabla ya nchi zengine kufuatilia katika miaka ya tisini).
1985-1990: Mbunge Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,
1985 – 1986: Naibu Waziri wa Fedha – Wizara ya Fedha , Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT).Msaidizi mkuu wa Waziri wa Fedha .kushughulikia masuala ya Uchumi na Mipango , matumizi na mapato ya Taifa pamoja na vyombo vya fedha .
1986 – 1989: Waziri wa Nchi , Wizara ya Mambo ya Nje, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT) anaesimamia Uhusiano wa Kimataifa na wa Kikanda, na vyombo vya Kimataifa na vya kiuchumi kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Afrika (OAU) na Tume ya pamoja Mashirikiano na nchi marafiki. 
Mwenyekiti katika kipindi chote wa Kamisheni hizo (Joint Commissions) na nchi zote marafiki za Afrika, Bara la Asia kama China, Iran, Urusi, Korea ya Kaskazini, Nchi za Marekani ya kusini kama Guyana, Venezuala, Ulaya ya Mashariki (Bulgaria). 
Mwenyekiti wa Vikao vya Mawaziri vya Kanda ya PTA sasa COMESA mwaka 1987, na Vikao vya Mawaziri wa SADC mwaka 1988. 
Mwenyekiti wa Kikao cha Mawaziri wa Fedha na Uchumi cha UNECA mwaka 1987 Ethiopia na Niger. Mwakilishi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye vikao vya G77, Mahusiano ya kiuchumi na nchi za Kusini (South South Cooperation) UNECOSOC, na Mwakilishi kwenye vikao vya nchi za Visiwa.



1989 – 1990: Waziri wa Nchi, Wizara ya Fedha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) Kushughulikia Mahusiano ya Kimataifa na Kikanda na pia kuratibu suala la kulipa madeni tunayodaiwa na nchi marafiki walio nje ya utaratibu wa Paris (IMF, WORLD BANK).
1990 – 2000: Mbunge Bunge la Jamhuri ya Muungano.
1990 – 2000: Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuteuliwa na Rais na pia Jimbo la Kwahani Zanzibar.

1990 – 2000: Waziri wa Fedha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwa na jukumu la kusimamia Uchumi wa Nchi Msimamizi Mkuu wa Sera ya Mapato na matumizi ya SMZ, Sera za Uchumi na Fedha na ukuaji wa Uchumi na vyombo vya Fedha zikiwemo Mabenki na Mashirika ya nayo husiana.

2001 – 2005: Mjumbe wa Tume ya Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar . Majukumu ya kusimamia sera za Uchumi ya Zanzibar na masuala yote ya Serikali yanayohusu Mipango ya nchi.
2005-2006: Mjumbe Baraza la Wawakilishi – nilijiuzulu baada ya kujiunga na AU.


2005 – 2006: Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kushughulikia uratibu wa Serikali, Tume ya Uchaguzi, Baraza la Wawakilishi, Sera ya Uwezeshaji wa wananchi na Mashirika yanayotoa mikopo midogo midogo TASAF, Mkurabita nk. Uratibu wa mashirikiano na Serikali ya Muungano (SMT), Masuala ya Maafa, Masuala ya walemavu, Masuala ya HIV-Aids na Tume ya Ukimwi ya Zanzibar na Uratibu wa mambo ya ndani ya Nchi Polisi na Uhamiaji.

Amb Amina Salum akisalimiana na Rais wa Marekani Bw. Obama.
2006 – Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) Marekani (United States) akiwa kama ni Muwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.
 (i) Mshauri wa Kamisheni Umoja wa Afrika kuhusiana mambo ya Afrika huko Marekani. (ii) Kufuatilia mambo ya Maendeleo ya Afrika huko Marekani kwa kuwajuilisha kuhusu sera mbali mbali za bara la Afrika zinazoendelea na mpya. (iii). Kuwashajiisha wawekezaji wa Marekani na pia Diaspora wa jamii ya Kiafrika huko Marekani kuwekeza Afrika.
 (iv) Kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na vyombo vya Serikali, Mabunge na Taasisi za kijamii za Afrika . 
(v) Kusaidia kupatikana kwa Fedha za Maendeleo ya Afrika kwa kuzieleza Sera za Maendeleo za Afrika, na kuwashawishi waziunge mkono.
 (vi) Kushirikiana na vyombo vya fedha vya Bretton Woods (World Bank na IMF) kwa Maendeleo ya Afrika. 
(viii) Kuleta mashirikiano na vyombo vya Elimu ya juu, Mashirika ya Kimataifa, Mifuko ya Maendeleo, Vyombo vya kujitolea na vya hiari (Universities, Research Institutes, Philanthropic Institute Foundations ie Gates, Clinton etc) Kuifahamisha Marekani mambo ya Maendeleo na taarifa njema za kutia moyo na zenye kuleta Maendeleo kwa jamii ya Afrika kwa wamarekani, kwa kutumia vyombo vya habari vyenye Taarifa sahihi.
(xv) kuratibu shughuli za ofisi za kibalozi za Afrika kwa lengo kubwa la kuweza kuwa na sauti ya pamoja katika masuala muhimu ya Afrika na maendelo yake pia na mahusiano na serikali ya Marekani.
UZOEFU KATIKA CHAMA:
1968: Nilijiunga na Umoja wa Vijana wa ASP (ASP Youth League) na kuendelea na Uanachama hadi kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977
1977: Nilijiunga na Chama Cha Mapinduzi baada ya kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM.
1987 – 2006: Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi hadi nilipolazimika kujiuzulu kufuatia kuteuliwa kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) huko Marekani. Mlezi wa Jumuiya ya Vijana Mjini.
1992 – 2006: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi hadi nilipojiuzulu kufuatia kujiunga na Umoja wa Afrika (AU).
2003 – 2006: Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wanawake ya Chama cha Mapinduzi , nafasi niliyolazimika kujiuzulu baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Umoja wa Afrika Marekani.
1987 – 2006: Mjumbe wa Kamati mbalimbali zilizoundwa na Chama kwa kipindi chote nilichokuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi.
Mlezi wa mkoa Morogoro.
Mlezi wa umoja wa vijana Zanzibar wilaya ya Mjini.
SHUGHULI ZA KIJAMII:
1990: Mwanzilishi wa Jumuiya isiyo ya Kiserikali (NGO) ya kwanza kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake (Catalyst Organisation for Women Progeress in Zanzibar).
1995: Mwanzilishi wa Zanzibar Welfare Trust, na pia nimekuwa mlezi wa Zanzibar NGO Clusters. Aidha nilkuwa Mwanzilishi wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
Mwanzilishi wa mfuko wa Rais wa Kujitegemea.
BODI MBALIMBALI:
1992 – leo Mwenyekiti wa Jumuiya isiyo ya Kiserikali ya kuendeleza Wanawake Zanzibar (Catalist Organisation for Women Progress in Zanzibar) –COWPZ.
1992-1995 Mjumbe Bodi ya Biashara za nje Wizara ya Biashara na Viwanda SMT.
1996 – 1999: Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Magazeti ya Chama Uhuru na Mzalendo.
2002- 2005: Mjumbewa baraza la chuo kikuu Cha mzumbe (Mzumbe university council),
2003 – 2004: Mjumbe wa Bodi ya Biashara ya Nje, Wizara ya Biashara na Viwanda – Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
2003 – 2005: Mjumbe wa Mfuko wa Elimu Zanzibar, Wizara ya Elimu Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar.
2004 – 2005: Mjumbe wa Bodi maalum iliyoshughulika na kazi za Maendeleo ya Wanawake katika Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (JEDDAH).
2004 – 2006: Mdhamini wa Jumuiya zisizo za Kiserikali Zanzibar (Zanzibar NGO Clusters – ZANGOC zinazoshughulika na masuala ya Ukimwi (HIV – AIDS).
LUGHA: Kiswahili na Kiingereza – Kuongea na Kusoma kwa Ufasaha.





Mama: Amina Salum Ali
 Mwanamke anaefaa  kuingoza Tanzania.
                                                                
Kuchukua  -fomu-za-kugombea-urais-wa-Zanzibar-mwaka-2000-kupitia CCM Zanzibar

Mkutano wa  hadhara wa-kampeni-Jimbo-la-Kwahani-1995.
Mama Amina akipokea  zawadi baada ya kukamilisha kuizindua NGO - Catalyst Organisation for Women Progeress in Zanzibar.
 Picha kamili ya Catalyst Organisation for Women Progeress in Zanzibar.


Mama: Amina Salum Ali

No comments:

Post a Comment