Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akichangia majadiliano kuhusu ajenda ya Maendeleo ya Jamii katika Mkutano wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati Sita zinazounda Baraza hilo zimeanza mikutano yake ikiwa ni wiki moja tangu kukamilika kwa mikutano ya Kilele ya Viongozi wa Kuu wa Nchi na Serikali iliyofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum, New York
Ikiwa
ni Wiki moja kupita tangu Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa mbalimbali Dunia,
kuhitimisha ushiriki wao katika
mikutano muhimu mikuu miwili, upitishwaji wa Malengo
Mapya ya Maendeleo Endelevu na Mkutano
wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Nchi wanachama wameingia katika hatua nyingine ya mikutano ya Kamati
Sita zinazounda Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa.
Kamati
zinazounda Baraza Kuu na ambazo
zimeanza
mikutano yake kuanzia
jumanne na itakayo kwenda hadi mwezi desemba kwa baadhi ya Kamati , ni Kamati ya Kwanza ambayo baadhi
ya majukumu yake ni pamoja na
udhibiti wa matumizi holela ya silaha za aina mbalimbali zikiwamo silaha
za nyukilia , kemikali, silaha ndogo ,
kubwa na nyepesi , upokonyaji wa silaha na masuala yahusuyo ulinzi
na usalama
Mikutano
ya Kamati ya pili nayo imeanza,
kamati ya pili inahusika na masuala yote ya uchumi, ikifuatia na Kamati ya
Tatu inayohusika na masuala ya
maendeleo
ya Jamii, Utamaduni na
Haki za Binadamu. Imeanza
pia mikutano ya Kamati ya Nne inayohusika na masuala
ya
kumaliza ukoloni,
operesheni za ulinzi wa Amani na
Kamati nyingine ambazo zinaunda Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
ni Kamati ya Tano ambayo inahusika na masuala ya Bajeti
na Utawala ikifuatia na Kamati ya Sita
inayohusika na masuala ya, pamoja na mambo mengine, sheria za kimataifa,
utawala wa sheria na mahakama za kimataifa.
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia Uwakilishi
wake wa Kudumu, inashiriki vema katika mikutano na mijadala yote ya Kamati hizi, ushiriki
ambao pia unawahusisha wataalamu wa fani na kada mbalimbali
kutoka Wizara na Idara za
pande zote mbili za Muungano.
Akichangia majadiliano ya Kamati ya Tatu kuhusu ajenda ya Maendeleo ya Jamii,moja ya kati ya ajenda
zitakazojadiliwa na Kamati
hii, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania
imendelea na jukumu la kuhakikisha
kwamba hakuna mtu wa rika lolote
anayeachwa nyuma katika ajenda hiyo.
Akasema
kuwa baadhi ya mikakati inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya
Muungano ni pamoja na
kuhakikisha kwamba
makundi yote ya jamii,
yanapata
fursa na haki ya kushiriki
katika utoaji wa maamuzi wa mambo yanayowahusu.
Balozi
Mwinyi, amefafanua kwa kutoa mifano
kadhaa
ya kisera na kiutendaji
na jumuishi inayolenga katika
kuwanufaisha na kuboresha maisha ya
vijana, wazee,
wanawake, watoto
wa kike, na makundi mengine ya jamii kama vile watu wasiojiweza.
Akaeleza kuwa
sera na mikakati hiyo inayolenga katika
kumwondoa mtanzania katika umaskini ni pamoja na mipango ya
uboreshaji na uendelezaji wa sekta mbalimbali
ikiwamo ya kilimo inayojari
watanzania wengi, uboreshaji wa sekta ya
elimu na miundo mbinu yake kwa kuongeza bajeti,
upatikanaji wa huduma za afya na
kwa gharama nafuu hususani kwa wazee na watu wasojiweza.
Balozi
Mwinyi ameeleza pia kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanya
kila iwezalo katika kuhakikisha
kwamba kila mtoto wa kitanzania
anapata fursa ya kupata elimu na si bora elimu lakini kwa kuhakikisha kwamba
elimu anayopewa ni bora na yenye viwango vinavyo kubalika kitaifa na kimataifa.
No comments:
Post a Comment