Habari za Punde

Dk Shein amuapisha Mkuu wa Wilaya ya Wete

 Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu]
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu]
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akisalimiana na kumpongeza Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo baada ua kuapushwa katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw. Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,kabla ya uteuzi huo Mkuu huyo  alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba,[Picha na Ikulu]


STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                13 Januari, 2015
---

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Bwana Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete katika mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Rashid alikuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Chake Chake katika Mkoa wa Kusini Pemba.

Hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Haji Omar Kheri, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji Khamis, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdulla Mwinyi na Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib.

Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.