Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Kukomalia Ujenzi wa Maegesho Jijini Mwanza

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus 

Mabula (CCM, ameahidi kushughulikia suala la ujenzi wa              

maegesho ya magari makubwa ya mizigo nje ya jiji la Mwanza ili 

kuzuia magari hayo kuingia katikati ya jiji.                                    

Akizungumza ofisini kwake hii leo, Mabula amebainisha kuwa        upo mpango wa kujenga maegesho hayo katika maeneo yaliyo nje 
ya Jiji la Mwanza, hatua ambayo itasaidia magari hayo kutoingia katikati ya Jiji na hivyo kuondoa malalamiko yaliyopo kutoka kwa madereva wa magari madogo ya mizigo wanaolalamikia uingiaji wa magari makubwa ya mizigo katikati ya jiji.                            

Ameyataja maeneo yanayotarajiwa kujengwa maegesho hao kuwa 

ni Buhongwa pamoja na Igoma na kwamba baada ya ujenzi wake 

kukamilika, magari yote makubwa ya mizigo hayataruhusiwa        

kuingia katikati ya Jiji.                                                                       

Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika     

uongozi uliomalizika mwaka jana, amebainisha kuwa utekelezaji   

wa ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kufanyika kwa uharaka 

zaidi ambapo amewahimiza wawekezaji mbalimbali kujitokeza ili 

kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya               
 kufanikisha ujenzi huo.                                                                       

Suala la magari makubwa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza huku 

yakiwa na mizigo, linalalamikiwa na madereva wa magari madogo 

ya mizigo kwa kile wanachoeleza kuwa wanaingiliwa katika           

shughuli ambazo wao wangezifanya na hivyo kujiingia kipato         

ambapo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoruhusu 

magari hayo kuingia katikati ya Jiji.                                              
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari ofisini kwake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.