Habari za Punde

Makocha wa Timu za Mafunzo na AS Vita ya DRC Wajigamba Timu zao Zitafanya Vizuri katika Mchezo wao wa Kwanza Utakaofanyika Zanzibar. Jumamosi.


Kocha Mkuu wa Timu ya AS Vita Club ya Congo Kiadivila -Zico akizungumza na waandishi wa habari za michezo kuhusiana na mchezo wao wa michuano ya Kombe la CAF unaotarajiwa kufanyika Zanzibar katika Uwanja wa Amaan Zanzibar wakiwa katika hali ya afya nzuri na wote wako safi hakuna majeruhi wanachosubiri nu ushindi siku ya mchezo wao huo wa awali.Na leo jioni wachezaji wake watafanya mazoezi mepesi katika uwanja wa amaan Zanzibar Timu imewasili leo mchana ikitokea Congo..
 Kocha Mkuu wa Timu ya Mafunzo Abdalla Bakar EDO akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchezo wao na Timu ya AS Vita ya Congo unaotarajiwa kufanyika jumamosi katika uwanja wa amaan Zanzibar na kuwaahidi wapenzi wa mchezo wa soka Zanzibar kujitokeza kwa wingi kuja kuishanguilia timu yao na kuongezea wachezaji wake wote wako fiti na wanaendelea na mazoezi yao kwa ajili ya mchezo huo na wachezaji wake wana ari kubwa ya ushindi.
 Waandishi wa habari za michezo Zanzibar wakifuatilia mkutano huo wa Makocha wa timu hizo mbili uliofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Amaan wa VIP Amaan Zanzibar.
 Viongozi wa timu ya Mafunzo wakiwa katika mkutano huo wa Makocha wa Timu hizo mbili wakitowa maelezo yao kwa Waandishi wa habari za Michezo Zanzibar
Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya ZFA Mwalim Masoud Atai akizungumza na waandishi wa habari za Michezo Zanzibar kwa kukamilika kwa mchezo wa Kombe la CAF kati ya Mafunzo na AS Vita ya Congo zimekamilika kwa asilimia mia moja katika matayarisho yake. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.