Maafisa wa kamati ya
Ulinzi na Usalama Mkoa Kusini Pemba, wakisubiri usafiri wa kuvukia kwelekea
kisiwa Panza, kusikiliza matatizo ya wananchi yaliyopelekea kutokuvuushwa kwa
baadhi ya wananchi wanaishi kisiwa hicho.
Viongozi mbali mbali
wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa kusini Pemba, wa kiongozwa na Mwenyekiti
wa kamati hiyo Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla
wakiwasili katika kisiwa Panza kwa boti ya Kikosi cha KMKM.
Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla akiwa
katika harakati za kutaka kushuka katika faiba ya KM KM baada ya kuwasili
katika kisiwa Panza kutoka Chokocho, kwa lengo la kuja kutatua mzozo
uliopelekea baadhi ya wananchi kutokuvuushwa kwa madai ya kisiasa
Wananchi wa Kisiwa
Panza Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
Mkao kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdall, wakati alipokuwa akizungumza nao
kufuatia baadhi ya wananchi kukataliwa kuvushwa kisiwani huko kwa madai ya
itikadi za kisiasa
Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba Mhe: Mwanajuma Majid Abdalla akiwa na
viongozi mbali mbali wa serikali katika kisiwa Pemba, kwa lengo la kukagua
mazingira ya kisiwa hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akitoa
maelezo kwa wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa kusini Pemba, wakati
walipowasili katika kisiwa Panza kusikiliza matatizo yaliyopelekea baadhi ya
wananchi kutokuvuushwa kwa madai ya kisiasa.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
haya wapemba sasa leteni fyoko fyoko
ReplyDeleteTengeneza dau lako tu uvuukie
ReplyDelete